-Siyo
siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba
na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya
fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015
-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr.
Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu
kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini
vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar
aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh
700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu,
thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January
Makamba?
-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba
jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima
akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye
kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie
tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa
hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo
-Naitahadharisha chama changu CCM
kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao
wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola
kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili
tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga
mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka
miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado,
kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.
-January hajawahi kuchaguliwa kwenye
cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali,
yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya
Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee
Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga
itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa
jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?
No comments:
Post a Comment