KOCHA mpya wa Simba Zdravko Logarusic amewasili nchini majira
ya 2:15 asubuhi na Kenya Airways jana huku akitoa ahadi kemkem kwa mashabiki wa
klabu hiyo yenye makao makuu mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Logarusic raia wa Croatia ambaye awali alikuwa anaifundisha
Gor Mahia ya Kenya na kuisaidia kuchukua Ubingwa baada ya ukame wa miaka 18
amesema yeye falsafa yake ni ya kucheza
mpira wa kushambulia haraka wakitokea nyuma (Counter attack) kwani ndio wenye
kuleta matokeo mazuri.
Akizungumza baada ya kuwasili Logarusic ambaye anatarajia
kusaini mkataba wa miezi sita leo amesema kuwa hatafanya mabadiliko ya
wachezaji katika kikosi hicho zaidi ya kuhakikisha Simba inachukua ubingwa kama
alivyofanya kwa Gor Mahia.
“Mimi kazi yangu ni kujenga timu ili icheze mchezo wa
ushindani wenye kuonekana bayana hasa kufanya mashambulizi ya haraka kwani nategemea Simba itabadilika
na kutwaa ubingwa ili icheze kombe la mabingwa barani Afrika”, alijigamba
Logarusic kocha nayeonekana kuwa muongeaji sana.
Kocha huyo amefikia Rombo View hotel iliyoko Shekilango,
Urafiki ambako amefikia golikipa Yaw
Berko aliyesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miezi sita kuitumikia Simba katika
mzunguko wa pili wa ligi Kuu Tanzania bara.
Mara baada ya kufika hotelini na kupewa chumba na kupata
kifungua kinywa alikwenda moja kwa moja kukagua uwanja wa Kinesi ambao
unatumiwa na Simba kufanyia mazoezi na kuridhika nao japo alionekana kutaka
kupata uwanja mwingine ambao anautumia anapokaribia kuwa na mechi.
Pia ametoa mapendekezo ya kupata mechi ya kirafiki kila wiki
ili aweze kujenga timu yake katika ushindani wakati wote.
Kocha huyo alipokelewa na wajumbe watatu wa kamati ya
Utendaji wa klabu ya Simba wakiongozwa na Saleh Pamba, Swedy Nkwabi na Damian
Manembe na mashabiki waliokuwa kwenye Coaster tatu.
Logarusic amewahi kuzifundisha timu za King Faisal Babies FC Kumasi toka mwaka
2009/2010 na Ashanti Gold SC toka 2010 hadi 2012 zote za
nchini Ghana na baadae alichukuliwa na
Gor Mahia ya Kenya toka Aprili 2012 hadi
Novemba 2013.
No comments:
Post a Comment