Saturday, May 22, 2010

Bouazza ashangaa kutoitwa kikosi cha Algeria 2010 A.KUSINI



Bouazza ashangaa kutoitwa kikosi cha Algeria 2010

ALGIERS,Algeria

NYOTA wa timu ya Taifa ya Algeria, Hameur Bouazza amesema kuwa ameshutushwa kuachwa kwenye kikosi cha awali cha nchi hiyo ya kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia.

Awali mshambuliaji huyo wa Blackpool alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuitwa katika kiosi hicho lakini akatemwa licha kuwa mmoja wafungaji bora wapya nchini humo.

Hatua ya kutemwa mchezaji huyo ni kutokana na Kocha Rabah Saadane kuwaita wachezaji watatu waliokuwahi kuicherzea timu ya vijana ya Ufaransa jambo ambalo lilisababisha kukosena nafasi kwa ajili ya Bouazza.

"Sina kinyongo chochote na wachezaji wapya ila nimefadhaishwa na kocha," Bouazza aliiambia BBC Sport.
"Kocha hajamipigia simu wala kuja kuniona na kunieleza choichote kama mtaalamu kwani mara zote nimekuwa najituma kwa Algeria najisikia kama nipemigwa na gongo la kuchezea mpira wa magongo,"aliongeza

Bouazza alikuwa mmoja wa wachezaji waliocheza kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Misri katika mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia na pia ndiye aliyefunga bao la ushindi dhidi ya Ivory Coast katika mechi ya robo fainaa za Mataifa ya Afrika.


"Nimefanya nao kila kitu niliapswa kuwemo katika kikosi hicho lakini imeshindikana,"alisema nyota huyo.
Alisema kuwa kwa sasa amepona majeraha yake ya misuli yaliyokuwa yakimkabili tangu alipotoka Angola.
"Wachezaji wengine bado ni majeruhi lakini bado wameitwa na wanapatiwa matibabu na sidhani majeraha ya kwangu ni makubwa kuliko ya wao na nadhani bado naweza kucheza,"alisema mchezaji huyo.
Hata hivyo Bouazza alisema kuwa ataendelea kuinga mkono Algeria itakapokuwa nchini Afrika Kusini na akasema kuwa atawaunga mkono wachezaji weenzake wa kimataifa.

Katika michuano hiyo Algeria itakutana na England,Marekani na Slovenia katika mechi za kundi C.

No comments:

Post a Comment