Saturday, May 22, 2010
FIFA yakiri mauzo ya tiketi ni duni JOHANNESBURG,A.Kusini
FIFA yakiri mauzo ya tiketi ni duni
JOHANNESBURG,A.Kusini
OFISA mwandamizi wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA ameelezea kuchanganyikiwa kwao na kiwango cha mauzo ya tiketi za kuangalia fainali za Kombe la Dunia zilizouzwa kwa mashabiki barani Afrika.
Ofisa huyo,Jerome Valcke alisema jana kuwa jumla ya tiketi zilizouzwa katika nchi za Afrika ni nje ya Afrika Kusini ni 40,000.
Hata hivyo bodi hiyo ya michezo imekuwa ikishutumiwa kwa kushindwa kurahisisha upatikanaji wa tiketi barani Afrika huku tiketi nyingine zikilazimika kupatikana kwa njia ya internet.
Lakini pamoja na shutuma hizo Valcke ambaye amekuwa akizisifia fainali hizo alisema kuwa mauzo ya teketi barani Afrika ni mabovu na akasema kuwa anadhani FIFA itabidi kujiuliza tena kuwapa Brazil nafasi ya kuandaa fainali kama hizo mwaka 2014.
"Siyo kiwango ambacho unaweza kudhania wakati kuna timu nyingi zinazocheza fainali hizi kutoka Afrika," alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari nchini Afrika Kusini.
"Utaratibu tulioweka siyo mbadala kwa Afrika Kusini na Afrika,"aliongeza.
Alisema kuwa pia kuna matatizo ya usafiri wa anga kutoka nchi za Afrika kwenda Afrika Kusini.
Kwa upande wake Waziri wa Utalii nchini Afrika Kusini, Martinus van Schalkwyk alisema kuwa hadi sasa walionunua tiketi ni asilimia 76 chini ya matarajio.
Alisema kuwa hadi sasa ni watu 11,300 barani Afrika waliokwishanunua tiketi mbali na raia wa kigeni 230,000 .
No comments:
Post a Comment