Danny Williams atakiwa kustaafu ngumi
London, Uingereza
BONDIA wa ngumi wa uzito wa juu Danny Williams ametakiwa kujiuzulu katika mchezo huo ili kulinda heshima yake.
Williams mwenye umri wa miaka 36, alipoteza pambano lake la kuwania ubingwa dhidi ya Mwingereza mwenzie Derek Chisora, Katika raundi ya pili katika pambano lake la 51.
Promota wa ngumi Frank Warren alisema: ÒDanny alikuwa ni mpiganaji mkubwa. Ninatumaini kuwa atastaafu. Hajaonesha kuwa mzuri kwa sasa.
Katika mechi nyingine James DeGale alimtwanga Sam Horton na kutwaa ubingwa wa WBA uzani wa super-middle.
No comments:
Post a Comment