Tuesday, May 18, 2010

Khan afurahi kupigana Marekani



Khan afurahi kupigana Marekani

NEW YORK, Marekani

AMIR Khan amefurahi kwa kutimiza ndoto yake ya kupigana katika ardhi ya Marekani na kushinda mechi.



Khan amepanga kurudi tena kupigana tena baada ya wiki nane, baada ya kushinda Jumamosi mechi yake katika raundi ya 11 dhidi ya Paulie Malignaggi katika ukumbi wa Madison Square Garden mjini New York.



Sehemu ambazo zinatajwa kupigana mechi ijayo ya kutetea tena ubingwa wake wa WBA uzani wa light-welter ni mjini London katika uwanja wa O2 Arena na MEN Arena wa Manchester.



Makubaliano yanatarajiwa kuanza ili kuwezesha mechi dhidi ya Michael Katsidis, ambaye alimpiga Kevin Mitchell katika uwanja wa Upton Park Jumamosi.



Uwanja wa MEN uko wazi kwa tarehe zilipendekezwa, Julai 24 na Julai 31, huku O2 uko wazi kwa Jula 31.



Khan mwenye umri wa miaka 23, alipata karibia milioni 2 kwa mechi yake dhidi ya Malignaggi aliyocheza New York, pamoja na mapigano yake ya nyuma akusanya karibia paunini milioni 15.



Anataka kureje ulingo kwa haraka kabl ya kuanza kwa mwezi Ramadhan Agosti 11.



Baba yake Shah alisema: "Kama tutapata mechi katika tarehe hizo Amir atapigana tena, lakini anataka kupigana kabla ya kuanza Ramadhan na kisha wakati wa kipupwe.

No comments:

Post a Comment