Marquee
tangazo
Saturday, May 29, 2010
Inter yamng'ng'ania JOSE MOURINHO MPAKA KIELEWEKE
Inter yamng'ng'ania Mourinho
Rome, Italia
KLABU ya Internazionale, imesema haitakubali kumwachia kocha wake, Jose Mourinho kwenda Real Madrid bila ya kupambana.
Mabingwa hao wapya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, wamesisitiza kuwa hakukuwa na punguzo kwa kifungu kinachotaka kuvunjwa mkatana kwa euro milioni 16."
Real inadai kuwa Mourinho, atatambulishwa rasmi Jumanne lakini kuwamekuwa na mvutano katika klabu hizo mbili, Real haitaki kutumia kufungu cha kuvunja mkataba ikizingatia kuwa jambo hilo linamhusu Mourinho na Inter.
"Sifikiri kama inaweza kutatuliwa katika saa 24, lakini inawezekana tukamtambulisha Mourinho kwa vyombo vya habari wiki ijayo.
Ninaweza kusema Jumanne," Meneja mkuu wa Real, Jorge Valdano aliiambia Radio Nacional.
Wakala wa Mourinho alikutana kwa mara nyingine na Inter Alhamisi, lakini hakuna ufumbuzi ambao ulipatikana.
"Kifungu cha kuvunja mkataba ni euro milioni 16 na hakutakuwa na punguzo," alisema Mkurugenzi wa Nerazzurri, Marco Branca wakati akizungumza na Sky Sport Italia.
"Hatujashangaa kitendo cha Real kusema kuwa watamtambulisha Mourinho. Hatuna haraka na hii si siku ambayo itatatuliwa."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment