Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 21, 2010

WALIOTAKA KUFUGA NDOA YA JINSIA MOJA WATUPWA RUPANGO

Waliotaka kufunga ndoa ya jinsia moja jela miaka 14 na kazi ngumu
BLANTYRE,Malawi

JAJI nchini Malawi amewahukumu kifungo cha miaka 14 jela pamoja na kazi ngumu wanaume wawili waliotaka kufunga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja baada ya Mahakama kuwatia hatiani mwanzoni mwa wiki hii.

Hukumu hiyo ilitolewa jana baada ya Mahakama mjini Blantyre kuwakuta na hatia watuhumiwa hao kwa kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo vimepigwa marufuku nchini humo.


Bw. Steven Monjeza, (26), na Bw. Tiwonge Chimbalanga, (20) walikuwa jela tangu walipokamatwa mwezi Desemba mwaka jana baada ya kufanya sherehe ya kuvalishana pete ya uchumba kabla ya kufunga ndoa yao iliyopangwa kufanyika mwaka huu.

Kukamatwa kwa wachumba hao kulizua kelele nyingi kutoka jumuiya za kimataifa na marumbano mengi kuhusu vitendo vya ushoga nchini humo.
"Nitawapa hukumu inayostaili ili kuilinda jamii kuondokana na watu kama wewe adhabu hii inaonesha kuwa hatupendi kuiga vitendo kama hivi," alisema Jaji Judge Nyakwawa Usiwa-Usiwa.
Kabla ya kutolewa hukumu hiyo mawakili waliokuwa wakiwatetea walitaka watuhumiwa kupewa adhabu nyepesi wakisema kuwa kitendo cha wachumba hao hakikumuathiri mtu yoyote.
"Siyo kama kosa la kubaka,hakuna mlalamikaji ama mwathirika katika kesi hii,"alisema wakili huyo baada ya watuhumiwa hao kutiwa hatiani Jumanne wiki hii.
"Hawa ni watu wawili wazima ambao waliamua kufanya jambo hilo binafsi na hakuna aliyetishiwa ama kutendewa makosa kama yange kuwepo yangesemwa hadharani,"aliongeza.(BBC)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...