Saturday, May 22, 2010
Keegan aitahadharisha England
Keegan aitahadharisha England
LONDON,England
KOCHA wa zamani wa timu ya Taifa ya England, Kevin Keegan ametahadharisha kuwa kikosi chake hiyo cha zamani hakitakuwa na nafasi yoyote katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia endapo mshambuliaji Wayne Rooney ataendelea kuwa majeruhi.
Tangu mwishoni mwa msimu uliopita mshambuliaji huyo wa Manchester United amekuwa akikabiliwa na majeraha ya enka na misuli na Keegan anasema kuwa endapo ataendelea kuwa katika hali hiyo litakuwa pigo kubwa kwa kocha wa sasa wa England, Fabio Capello katika jitihada zake za kutwaa ubingwa huo.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha tekevisheni cha Bloomsberg kocha huyo alisema kuwa endapo England itapoteza wachezaji wengine halitakuwa pigo tu bali litakuwa ni balaa kubwa.
"Endapo England itampoteza Rooney naweza kusema haitakuwa na nafasi, kwa sasa ni mmoja wa wachezaji ambaye anaweza kufanya maajabu ndani ya timu,"alisema.
"Kila mmoja atakuwa na wachezaji muhimu na kwa upande wetu ni Rooney na nadhani kama atacheza vizuri na kucheza katika kiwango chake basi England inaweza kufika nusu fainali,"aliongeza.
Keegan, ambaye aliiongoza England katika mechi za kufuzu fainali za Mataifa ya Ulaya za mwaka 2000 vilevile alimsifu kocha Capello lakini akamuaonya kuhusu kasheshe linaloweza kumkuta endapo timu yake itavurunda nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment