Buffon: Tutashangaza wengi
ROME,Italia
MLINDA mlango wa timu ya Taifa ya Italia,Gianluigi Buffon anaamini kikosi hicho cha Azzurri kinaweza kufanya maajabu katika mechi za fainali za Kombe la Dunia licha ya kuwa hakuna hata mmoja anayewapa nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
"Nadhani kikosi hiki ni kama cha miaka yote,tutaanza taratibu," Buffon aliliambia Shirika la Habari la ANSA. "Watu wengi hawadhani kama tutafanya vizuri lakini mwishoni naamini tunaweza kufanya hivyo,"aliongeza.
Alisema kuwa kikosi chao kitaongoza kundi lao na kitashangaza wengi katika mashindano hayo kama ilivyotokea nchini Ujerumani miaka minne iliyopita.
Mechi ya kwanza ya Italia itakuwa ni dhidi ya Paraguay ambayo itafanyika Juni 14 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment