Sunday, May 23, 2010

Milito shujaa, Mourinho ampiku bosi wake



Milito shujaa, Mourinho ampiku bosi wake

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Inter Milan ya Italia, Diego Alberto Milito jana aliibuka shujaa katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuifungia timu yake mabao mawili dhidi ya Bayern Munich katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid Hispania.

Mabao yao ya MIlito yaweza kuipa ubingwa timu yake na kujinyakulia kitita cha sh. bilioni 14 za Kitanzania huku kocha wake Jose Mourinho akimdhihirishia bosi wake kocha wa Bayern, Louis Van Gaal kuwa sasa amekua.

Mchezo huo ambao ulikuwa na kila aina ya ushindani huku kila timu ikisaka ushindi lakini ilikuwa ni bahati kwa Inter ambayo ilikuwa ikitumia staili ya kuzuia zaidi na mashambulizi ya ghafla.

Milito hakufanya makosa dakika ya 34 baada ya kuwainua mashabiki wa timu yake akimalizia pasi safi iliyopigwa na Wesley Sneijder aliyepokea mpira wa kauntaataki uliopigwa na kipa wao David Villa.

Kipindi cha pili Bayern walianza kwa kasi kwa wakitaka kupata bap la kusawazisha lakini wataijutia nafasi waliyopata dakika ya 48 lakini wakashindwa kuitumia.

Wakati Bayern wakisaka bao la kusawazisha wajikuta wakipigwa bao la pili dakika ya 70 liliofungwa na Milito tena baada ya kumlamba chenga beki wa Bayern Daniel van Buyten akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Samuel Eto'o.

Bao hili lilimwinua Mourinho katika kiti chake lakini baada ya kushangilia aliwatuliza wachezaji wake akiwa na maana kuwa kazi bado inaendelea hivyo watulie.

Pamoja na jitihada za Bayern kusaka mabao ya kusawazisha lakini hadi kipenga cha mwisho matokeo yalibaki kama yalivyo na Bayern kuambulia kitita cha sh. bilioni 8 za Kitanzania.

No comments:

Post a Comment