Saturday, May 22, 2010

Carragher: Siwezi kukataa woto wa Capello


Carragher: Siwezi kukataa woto wa Capello

LONDON,England

BEKI wa Liverpool, Jamie Carragher amesema kuwa hasingweza kukataa wito wa kocha Fabio Capello wa kumuita arejee katika kikosi cha England na akasema kuwa kwa sasa anapigania nafasi hiyo ya kwenda kucheza fainali za Kombe la Dunia.
Baada ya kustaafu kuchezea timu ya Taifa miaka mitatu iliyopita Carragher amerejea katika kikosi hicho akiwa na matumaini atakuwa miongoni mwa wachezaji ambao Capello atawachagua kwernda nao Afrika Kusini wiki chache zijazo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 akiri kuwa hakutarajia kuichezea tena England lakini baada ya kuona Capello akiichukua timu mwaka 2007 kutoka mikononi mwa Steve McClaren alifikiria upya kustaafu kwake.

"Nilifanmya maamuzi miaka michache iliyopita kwa sababu tofauti," Carragher alikaririwa na Shirika la Habri la Uingereza AP.
"Lakini nafasi hii ya kujaribu kuingizwa katika kikosi cha wachezaji 23imekuja tena siwezi kuitema na kocha Fabio Capello ni mmoja wa makocha wazuri na siyo kwa timu ya Taifa ya England ila kwa ulimwengu mzima zaidi ya kipindi cha miaka 10 ama 15 iliyopita,"aliongeza katika mahojiano hayo na AP.

Alisema kuwa mara zote amekuwa akimuuliza Steven Gerrard kitu ambacho kocha anakihitaji pindi atakapotaka kurejea katika majukumu ya kuichezea England na kasema kuwa huenda hiyo ndiyo sababu iliyopoa nyuma ya kuitwa kwake.

Inaelezwa kuwa kabla ya kuitwa katika kikosi hicho kwa mara ya kwanza Carragher aliwasiliana na kocha msaidizi wa England, Franco Baldini miezi michache iliyopita kutokana na kuwepo kwa hali ya wasiwasi kuhusu afya za wachezaji Joleon Lescott na Wes Brown.
Na baada ya mabeki wote wawili kutemwa kwa ajili ya fainali hizo ndipo Baldini aliwasiliana tena na mkongwe huyo wa Liverpool kufikiria tena uamuzi wake jambo ambalo Carragher alilikubali.

No comments:

Post a Comment