Thursday, May 20, 2010
UDSM MABIGWA WA KWANZA WA MCHEZO WA POOL WALIVYOTOA UBWINGWA UHO
MABINGWA WA KIHISTORIA WA MCHEZO WA POO UDSM WAKIWA NA KIKOMBE
MMOJA WA WASHIRIKI WA MICHUANO YA POOL AKIJITAARISHA KUPIGA MPIRA
Wasomi waing'arisha Pool
* Waonesha kiwango cha hali ya juu
* Wawatia hofu wachezaji timu ya Taifa
Na Erasto Stanslaus
MCHEZO wa Pool kwa kipindi kirefu kumekuwa na tafsirikuwa unaochezwa na walevi, kutokana na mchezo huo kuchezwa kwenye mabaa sana.
Lakini mwishoni mwa wiki hii, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager waliondoa dhana hiyo baada ya kudhamini mashindano ya Pool kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na vya Kati vya Dar es Salaam.
TBL wakishirikiana na Chama cha Pool Tanzania (TAPA) waliyabatiza jina mashindano hayo kuwa ni High Learning Safari Championship, ambayo yalishirikisha vyuo 16 vya jijini.
Mashindano hayo ya aina yake yalianza kutimua vumbi Mei 14 hadi 16 ambapo yalimalizia kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuibuka kidedea na kuwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo, wakifuatiwa na Chuo cha Biashara cha CBE na mshindi wa tatu kilikuwa chuo cha Ustawi wa Jamii.
Lengo la TBL ni kuufikia mchezo huo katika anga ya juu zaidi ikiwa pamoja na kutambulika ndani na nje ya nchi na sambamba na kuondoa dhana hiyo potofu inayoaminika kwa jamii.
Mashindano hayo ambayo yaliendeshwa kwa mtindo wa mchezaji mmoja mmoja kwa wa kike na kiume pamoja na mtindo wa timu.
Katika mtindo wa timu vyuo hivyo viligawanyika katika makundi mawili huku kila kundi likiwa na timu nane ambazo zilichuana na kupata timu nne zilizotinga nusu fainali.
Kundi A lilikuwa na timu za vyuo vya UDSM, RCT, Dar Star College, IMTU, Tumaini, Ustawi wa Jamii, DSJ na DIT, kundi B lilikuwa na timu za CBE, Chuo Kikuu Huria, TSJ, Mwalimu Nyerere, IFM, TIA, ITA na Chuo Kikuu cha Ardhi.
Katika kundi A timu zilizopenya katika nusu fainali ni UDSM na Ustawi wakati Kundi B zilipita timu za ITA na CBE ambazo ziliiumana vikali na kumpata mshindi ambaye ni UDSM.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja, walijitokeza wasomi 47 kutoka katika vyuo hivyo 16 ambao walichuana vikali katika mtindo wa mtoano hadi kumpata mshindi kwa upande wa wanawake na wanaume.
Kutokana na viwango vilivyoonyeshwa na wasomi hao zilidhihirisha kuwa mchezo huo unawigo mpana ambao kwa juhudi zinazowekwa, mchezo huo utakuwa tishio na utafika mbali.
Kupitia mashindano hayo ambayo Meneja wa Bia ya Safari, Fimbo Butallah alisema ni mwanzo, yameonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata timu bora ya Taifa zaidi ya ile iliyopo sasa ambayo imeshiriki katika mashindano mbalimbali barani Afrika na Dunia.
Awali timu hiyo ya Taifa ilikuwa ikichaguliwa kupitia katika mashindano ya klabu bingwa ya Tanzania yanayoshirikisha mikoa yote, lakini kwa changamoto hii kuna uwezekano wasomi hao wakatoa wachezaji wazuri zaidi ya waliopo sasa.
Katika fainali hizo, Fimbo alisema kutokana na mwanzo wa michuano hiyo umekuwa mzuri na wa kuridhisha, atajitahidi katika juhudi zake za kuupeleka mchezo huo juu, mashindano hayo kwa sasa yatabeba sura ya nchi nzima.
"Tumepokea simu kutoka katika vyuo mbalimbali kutoka mikoani wakitaka mashindano hayo, hilo tumelikubali na sasa tutashirikisha vyuo mikoani na kumpata bingwa wa Tanzania," alisema Fimbo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alisema wasomi hao wameonesha kuwa wao ni wasomi kweli kwani mashindano hayo yameendeshwa kisomi.
"Mbali na viwango vilivyooneshwa na wasomi hao lakini pia wamecheza mashindano hayo kwa nidhamu ya hali ya juu ambao huwa ni adimu katika michezo mingine kupatikana, nawapongeza sana," alisema Bendera.
Bingwa katika mashindano hayo ambaye ni UDSM amejinyakulia kombe pamoja na kitita cha sh. milioni 1, wakati CBE wamepata sh. 600,000 na mshindi wa tatu, Ustawi wameambulia sh. 400,000.
Zawadi kwa washindi wa mchezaji mmoja mmoja, mshindi amepata sh. 200,000 wakati mshindi wa pili amepata sh. 150,000 na watatu amepata sh. 100,000, zawadi hizi ni kwa wanaume na wanawake.
TBL wameahidi kuboresha mashindano hayo ili kuongeza msisimko zaidi ikiwa pamoja na kutimiza malengo yao ya kupeleka mashindano hayo kwa vyuo vya nchi nzima.
No comments:
Post a Comment