Thursday, June 17, 2010

Ibragimov amtwanga McCall kwa pointi




HOLLYWOOD, Marekani

BONDIA Timur Ibragimov wa Uzbekistan ameshinda pambano lake la uzito wa juu duniani dhidi ya bingwa wa zamani wa WBC, Oliver McCall juzi.

Ibragimov alikuwa akijituma na kupiga ngumi za uhakika katika raundi zote 12, alishinda kwa alama 117-111 kutoka kwa majaji wawili na alama 119-109 kwa jaji wa tatu.

Ilikuwa ni pambano la kwanza kwa McCall, tangu alipokamatwa kwa kukutwa na dawa za kulevya Februari 13, mwaka huu mjini Fort Lauderdale.

McCall mwenye rekodi ya (54-10), katika raundi ya awali alirusha ngumi ya kushoto kichwani mwa Ibragimov, ambaye naye alijibu.

McCall mwenye umri wa miaka 45, alijitahidi kucheza vizuri katika raundi ya sita na saba kwa kurusha ngumi kichwani mwa Ibragimov.

Pia, Ibragimov mwenye rekodi ya (28-2-1), aliendele kurusha ngumi na kuendelea kupata alama katika raundi za mwisho.

Katika raundi ya tatu, Ibragimov mwenye rekodi ya (28-2-1), alichangamka kwa kurusha ngumi.

Ibragimov, aliyekuwa na uzito wa kilo 104, alicheza vizuri raundi ya tano, kwa kurusha ngumi ya kushoto na kulia kichwani mwa mpinzani wake mwenye uzito wa kilo 116 kilograms.

McCall ndiye alimaliza utawala wa awali wa Lennox Lewis, katika ngumi za uzito wa juu kwa kushinda raundi ya pili Septemba 1994.

Baada ya kutetea vizuri ubingwa wake kwa Larry Holmes Aprili 1995, McCall alipoteza taji kwa Frank Bruno miezi mitano baadaye.

No comments:

Post a Comment