Thursday, June 17, 2010

P DIDDY AKATAA KUNUNUWA CRYSTAL PALACE



LONDON, Uingereza

MWANAMUZI wa rap Diddy, ambaye awali alikuwa akifahamika kama P Diddy na Puff Daddy, amesema ni kweli alitaka kuinunua Klabu ya soka ya Crystal Palace, ambayo iko ligi daraja la kwanza.

"Kulikuwa na mtu ambaye alikuwa akifuatilia, lakini bishara ya aina hiyo haikuwa sahihi kwangu kwa wakati ule," mwanamuziki huyo aliliambia shirika la Utangazaji la Uingereza BBC.

Crystal Palace ilikuwa kwenya matatizo ya kifedha hadi iliponunuliwa wiki iliyopita na muungano wa kampuni za CPFC 2010.

Lakini Diddy alisema bado amekuwa akingalia Klabu ya soka ya kununua.

"Kila wakati ninaangalia biashara tofauti na wazi ni moja kati ya ndoto zangu, siku moja kuwa katika biashara ya michezo hasa soka," alisema.

"Kama hali nzuri itakuja katika njia yangu... tunaweza kuwekeza na kujenga timu nzuri na kushinda... niko katika ushindi na kama hali itakuwa nzuri hilo ninaweza kufanya."

Rapa huyo amekuwa akipata mapato ya wastani wa pauni milioni 21 (sawa na dola 30) kwa mwaka, kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Hivi karibuni Rapa huyo ataonekana kama Stering, sambamba na
Russell Brand katika filamu ya Get Him To the Greek, ambayo itakuwa hadharani Uingereza Juni 25, mwaka huu.

Pia anaendelea na sanaa ya muziki kwa kuanzisha kundi jipya liitwalo Diddy- Dirty Money, ambalo limetoa wimbo wao mmoja wa Hello Good Morning Jumatatu.

No comments:

Post a Comment