Sunday, June 6, 2010
KOCHA WA ASHANTI BOXINGI KUFUNDISHA NGUMI UFUKWENI
KOCHA WA TIMU YA NGUMI YA ASHANTI RAJABU MHAMILA SUPER 'D' AKIWA NA MWANAFUNZI WAKE ABDALLAH MAGONZA
Na Addolph Bruno
MDAU wa mchezo wa ngumi na Kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' ameanzisha programu maalumu ya kutoa mafunzo kwa mabondia wa kujitegemea wanaocheza mchezo huo katika eneo la ufukwe wa Klabu ya Gyhmkana ili kukuza maendeleo ya mchezo huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mhamila ambaye ni kocha mkuu wa Klabu ya ngumi ya Ashanti alisema programu hiyo itakuwa ikiendeshwa siku za Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 12 asubuhi.
"Hii ni Programu mpya ambayo mimi kama mdau wa ngumi na bondia wa siku nyingi nimeamua kujitolea kuwapa mafunzo mabondia wenzangu ambao wamekosa bahati ya kuwa na walimu na nafasi ya kushiriki mafunzo ya ngumi na nafanya bure," alisema.
"Lengo langu ni kuinua mchezo huu ambao umepoteza umaarufu wake kwa muda hapa nchini na naamini kwa kuanzisha programu mbalimbali kama hizi kwa kushirikiana karibu na jamii tutaweza kuufikisha katika hatua flani," aliongeza.
Alisema lengo la kuandaa mpango wake huo ni kutaka kuwaweka watu karibu na mchezo huo ili kuuweka katika sura mpya baada ya kupoteza umaarufu wake kwa muda hapa nchini.
Alisema anatoa mafunzo hayo anatoa bure kwa mtu yeyote mwenye ufahamu wa kutosha juu ya mchezo huo na kuwaomba watu ambao wamekosa bahati ya kupata mafunzo kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment