Monday, June 21, 2010

MAAJABU KATIKA KOMBE LA DUNIA 2010


Pamoja na kiwango kibovu na duni kilichoonyeshwa na mataifa vigogo katika ulimwengu wa soka Ufaransa, Hispania,Uingereza lakini kuna timu kama nne hivi ambazo zenyewe zimeonyesha maajabu na kubaki kushangaza ulimwengu kutokana nidhamu na kiwango cha mpira walichoonyesha katika kombe la Dunia 2010 huko Afrika kusini.

1. Korea ya kasikazini (North Korea) na kundi la Hatari

Timu ya Korea ya kasikazini pamoja na matatizo yao ya kisiasa imejizolea maelfu ya washabiki katika kombe la dunia baaada ya kuonyesha kiwango chake na vigogo wa soka Brazil ambapo walipata goli la kufutia machozi kupitia mshambuliaji wao Yi yun-Nam baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Mchezaji wao bora Jong tae se. Ambapo katika mechi hiyo wachezaji wenye majina makubwa kama Kaka na Luis fabiano walionekana kufunikwa kabisandani ya uwanja. Cheche zilizoonyeshwa na mchezaji Jong tae se zinaleta matumaini kwa kikosi hicho katika mecho zake zilizobaki kati ya Ivory cost na Ureno.

2. New Zealand walivyowaharibia rekodi Italia

Ni timu ambayo naweza kusema ina bahati katika kombe la dunia kwani ilipata point ya muhimu kupita sloveni ktk dk 93 baada ya kichwa safi kilichopigwa na mchezaji wao Winston Reid. Pamoja na hilo walionekana kuwa bado wako ktk kiwango kizuri baadaya kuwatibulia mabingwa watetezi wa kombe la dunia Italia na kutoka nao sare ambayo wastahili kwa kweli. Kuna vitu vitatu vya muhimu vimeonekana kuwasaidia Newzealand kuwashindwa vigogo hao navyo ni Mbinu nzuri , safu ya Ulinzi na bahati. Utaalamu wa walinzi Nelson na Vicelich wa New Zealand uliwafunga washambuliaji wa italia wakina Gilardino na Di Natalie na kuonyesha kuwa pamoja na kuwa wachezaji wasio maarufu wanaweza kubadilika na kulinganishw ana wachezaji maarufu duniani.


3. Uswisi wameandika historia katika medani ya michezo

Gelson Fernandes scores the shock opener

Ni kitu cha kujivunia kupata ushindi wa muhimu baada ya kuwabamiza mabingwa soka wa ulaya hispania kwa 1-0. Uswisi ambayo ilimiliki kidogo sana mpira kulinganisha na 74% ya hispania walijitahidi kuzuia mipira yote ya mashambulizi kuacha mabingwa hao wakitoka bila goli. Wamejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mashindano hayo kwani ushindi wa mechi ya kwanza ni muhimu katika timu yoyote.

4. Ufaransa hawana hata goli moja

Mabingwa wa dunia hawa wa mwaka 1998 wameonekana kutindikiwa na mawazo mengi kwani kikosi cha Mfaransa Domenech hakijafanikiwa kufumania nyavu hata mara moja katika mechi zao mbili walizocheza yaani bilabila na Uruguay na pia kufungwa 2 bila na Mexico. Hicho kipigo walichopata kutoka kwa Mexico kimewachanga vigogo hao wa soka kwani kimeacha kambi yao ikitikisika kwa migogoro kati ya wachezaji na kocha wao. Mgogoro uliopo sasa hivi kati ya wachezaji na Kocha wao umepelekea hadi mchezaji Nickolas Anelka (mchezaji wa zamani wa Arsenal na Real Madrid) kurudishwa nyumbani ufaransa na viongzi wa chama cha soka cha nchi hiyi FFF. Wakiwa wamegoma kuhudhuria mazoezi jana jumapili bado wana matumaini madogo ya kusonga mbele kwani wategemee upinzani kwa wenyeji wa mashindano hayo Afrika kusini. Uongozi wa soka akiwemo pia Raisi Wa Ufaransa Sarkozy amewaasa wachezaji hao kuwa na hali ya utulivu.

No comments:

Post a Comment