Monday, June 21, 2010

WANAWAKE WASHAULIWA KUJITOKEZA KATIKA MCHEZO WA POOL


CHAMA cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), kimewashauri wanawake nchini kushiriki mashindano mbalimbali ya mchezo huo ndani na nje ya nchi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TAPA, Amos Kafwinga alisema wanawake wameonekana kuwa nyuma katika mchezo huo na kuwataka wajitokeze kwa wingi kushiriki.

Alisema wanawake wamekuwa wamekuwa wakitoa lawama mara nyingi katika michezo mbalimbali wakati hawajitokezi kushiriki.

"Kwa muda mrefu tumekuwa tukiwashawishi wanawake kucheza pool, lakini hatujafanikiwa, Kamati ya Utendaji imependekeza kuanzisha mashindano yao," alisema.

Kafwinga alisema baada ya juhudi zao bila mafanikio, wamepanga kuanzisha mashindano hayo ambayo yatakuwa yanashirikisha wanawake pekee ambayo bado whawajajua ya.

Alisema mashindano hayo yatakuwa kampeni ya kuhamisha mchezo huo kwa wanawake ili waweze kuelewa kama wana nafasi kubwa ya kushiriki mchezo huo.

Katibu huyo alisema mchezo wa pool ni mchezo uliokuwa na sheria chache ambazo wanawake wanaweza kuzizingatia na kufanikiwa.

No comments:

Post a Comment