Wednesday, June 9, 2010

Mensah abeza mawazo ya timu za Afrika kutwaa ubingwa




JOHANNESBURG,A.Kusini

BEKI wa Ghana, John Mensah amepuuza mawazo ya kwamba kuandaliwa kwa michuano ya fainali za Kombe la Dunia katika ardhi ya Afrika inaimanisha kuwa timu kutoka bara hilo zitatwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Akipuuza mawazo hayo Mensah alisema kuwa kila timu ikiwemo Ghana zinatarajia kutafakari majaliwa yake wakti wa fainali hizo zitakazoanza kutimua vumbi nchini Afrika Kusini.

“Najivunia kucheza katika fainali hizi zinazofanyika kwa mara ya kwanza Afrika ,”aliliambia gazeti la The Journal.
“Lakini siyo kwa sababu kwamba zinafanyika Afrika inaimanisha kuwa timu za Afrika zinaenda kutwaa ubingwa.Hatuhitaji kuwaza hivyo kwa sababu tuna kitu ambacho kipo nje yauwezo wetu ila tunachohitaji kujifikria wenyewe,”alisema ambaye ni mara yake ya pili kuonekana katika fainali hizo baada ya zilizofanyika nchini Ujerumani mwaka 2006.
Wawakilishi hao mara sita kutoka Afrika wakiwemo wenyeji Afrika Kusini wanashiriki katika mashindano hayo.
Timu nyingine za Afrika zinazoshiriki ni Nigeria, Ivory Coast, Algeria, Cameroon na Ghana.

No comments:

Post a Comment