Tuesday, June 8, 2010
ZAIN KUITEKA A.KUSINI KATIKA KOMBE LA DUNIA
Zain, mtandao unaoongoza Barani Afrika imetangaza kwamba huduma yake kabambe ya One- Network imepanuka zaidi na kuingia Afrika Kusini kupitia ubia na kampuni ya simu ya Cell C ya Afrika Kusini.
Zaidi ya wateja milioni 41 wa Zain katika nchi zote 15 za Zain Afrika zenye mtandao wa Zain sasa watanufaika na huduma ya Zain ya One Network wakitembelea Afrika Kusini ikiwemo watu watakaoenda nchini humo kushuhudia fainali za Kombe la Dunia.
Huduma ya Zain ya One Network huwawezesha wateja wa Zain walio katika mpango wa malipo baada na wale wa malipo kabla kutozwa gharama kama za mteja wa ndani wakati wakipata huduma zote za nyumbani walikotoka.
Sasa wakiwa Afrika Kusini wateja wa Zain wataweza kupiga simu, kutuma sms na kuangalia data kwa viwango vya ndani ya nchi waliyotelembea na kupokea simu za mkononi kwa gharama ndogo.
‘’Tumefikia kilele cha mafanikio kwa kuweza kupanua huduma yetu ya One Network hadi Afrika Kusini, nchi inayoongoza Barani Afrika. Ambayo mwaka huu itakuwa kituo cha dunia cha michezo,’’ alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain Africa Chris Gabriel. ‘’One Network haina mpinzania, na katika kila nchi tunayosimika bendera ya One Network tunabadilisha maana ya mawasiliano ya simu za mkononi na dhana nzima ya Zuru za Kimataifa na kutekeleza ahadi yetu ya Ulimwengu Maridhawa wa Zain.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania Ahsan Syed amesema ‘’Tunavyokaribia kusherehekea Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Afrika, Zain kampuni inayoongoza kwa ubunifu imepanua huduma yake kabambe ya gharama nafuu ya One Network Afrika Kusini. Hatua hii inaenda sambamba na promosheni yetu ya kusisimua ambapo tutatoa tiketi 12 za kombe la FIFA kwa wateja wa Zain tukiwa tumewalipia gharama zote za usafiri na malazi,’’ alisema Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania Ahsan Syed.
‘’Wakiwa nchini Afrika Kusini, wateja wetu wataweza kutumia namba zao za Zain kupiga simu, kutuma SMS na kutumia huduma ya internet kwa viwango vya ndani, pamoja na kupokea simu kwa gharama nafuu,’’ alisema Syed.
Wateja hawahitaji kujisajili kabla ya kusafiri kwenda Aafrika Kusini, na kuweka amana, na hakuna kero katika namna ya kupiga simu. Kama katika nchi nyingi wateja wanaweza kuongeza muda wa maongeza kwa kutumia vocha za simu zinazipatikana Afrika Kusini.
“Urahisi ni moja ya maadili makuu ya Cell C, NA One Network inafanya huduma ya Zuru za Kimataifa kuwa rahisi zaidi wateja wa Zain. Tumefurahi kwamba tunawawezesha wageni wa Zain Afrika Kusini kutumia mtandao wetu kwa gharama ambazo wateja wa ndani wanatozwa,’’ alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Cell C , Lars P Reichelt. Kushirikiana na Zain kumeenda vizuri na tumefurahi kwamba bendera ya One Network pia ina rangi za taifa na rangi za Cell C.
Tangu kuanzishwa kwake Afrika Mashariki September 2006 na baadaye kupanuka hadi bara la Mashariki ya Kati, One Network imetambulika katika soko la kimataifa la simu za mkononi kama huduma ya ubunifu mkubwa iliyoweka viwango vipya katika mawasiliano kati ya mpaka mmoja na mwingine.
Nchi 15 zitakazo nufaika na huduma hii na Cell C nchini Afrika Kusini ni; Burkina Faso, Chad, Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Malawi, Madagascar, Niger, Nigeria, Sierra Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.
Kwa maelezo zaidi tembelea www.zain.com au barua pepe
No comments:
Post a Comment