Tuesday, June 8, 2010

SAFARI LAGER YATANGAZA UDHAMINI WA MASHINDANO YA MCHEZO WA POOL KITAIFA 2010


Katibu wa mchezo wa pool Taifa, Amos Kafwinga akizungumza na waandishi wa habari leo asubui kushoto ni meneja wa bia ya safari lager Fimbo Butallah

Mwenyekiti wa mchezo wa pool,Isaac Togocho kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuusu mashindano ya mchezo wa poo yatakayoanza mwezi ujao kulia ni Fimbo Butallah

Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano uho leo


Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kwa mara nyingine udhamini wake katika mashindano ya Taifa ya mchezo wa pool mwaka 2010 mashindano hayo yanatarajia kuanza rasmi tarehe 13 mwezi julai 2010 katika ngazi za mikoa
Akitangaza udhamini uho meneja wa bia hiyo Fimbo Butallah amesema'Bia ya SAfari Lagel' imekuwa mdhamini mkuu wa mchezo huu.hivyo ni dhamira ya bia hiyo kuendelea kudhamini mashindano haya ya taifa na mengine mengi mchezo wa pool hapa mchini.

Udhamini huu unaanzia ngzi ya mikoa hadi fainal ambazo kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika mjini Arusha mwishoni mwa mwezi Septemba 2010

Meneja huyo wa bia ya Safari aliongeza kuwa udhamini wa mwaka huu umeongezeka ukulinganisha na miaka ya nyuma.Ikiwa ni pamoja na ongezeko la mikoa shiriki na zawadi za washindi.Akiweka wazi aina ya zawadi ambazo washindi wa mwaka huu watapata katika ngazi za mikoa na taifa.Fimbo Butallah amesema bingwa 500,000 mshindi wa pili 250,000 na wa tatu ataondoka na kitita cha 150,000

No comments:

Post a Comment