Monday, July 12, 2010

ASAMOAH GYAN ATAKIWA NA KLABU YA SUNDERLAND


LONDON, Uingereza

KLABU ya Sunderland, imeinngia katika mbio za kutaka kumsaini mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan, ili kuwaunganisha wachezaji watatu wa nchi hiyo waliokuwemo katika michuano ya Kombe la Dunia Afrika Kusini.

Mshambuliaji huyo wa Rennes, ambaye alikosa penalti katika dakika za mwisho kwenye mechi ya robo fainali dhidi ya Uruguay Ijumaa, iliishia kwa kupigiana penalti, amekuwa akitajwa kutakiwa pia na West Ham.

Lakini Hammers imeonekana kusuasua wakati ambapo inamtaka mshambuliaji wa Loic Remy.

Kocha wa Sunderland, Steve Bruce amekuwa na bajeti ya kusaini wachezaji na inaweza kumudu kulipa dau la pauni milioni saba, linalotakiwa kwa ajili ya Gyan.

Bruce amekuwa ana matumini ya kuweza kumpata nahodha huyo wa Ghana, John Mensah, ambaye pia anatajwa kutakiwa na Hamburg, baada ya kucheza kwa mkopo kwa mafanikio na imeeleza nia ya kumpata mshambuliaji wa AC Milan, ambaye ni Mghana Dominic Adiyiah mwenye umri wa miaka 20.

Gyan ambaye alikuwa akicheza mbele kwenye kikosi cha Ghana, alimaliza michuano hiyo kwa kufunga magoli matatu na pia alifunga goli la penalti katika robo fainali.

Uchezaji wake mzuri umezifanya Klabu kadhaa kuwania saini yake.
Sunderland pia inashindana na West Ham kwa ajili ya kumpata mlinzi wa Algeria, Rafik Halliche mwenye miaka 21, ambaye anaweza kupatikana kwa ada ya pauni milioni 1.2 kutoka Benfica.

No comments:

Post a Comment