Monday, July 12, 2010

MABONDIA WA ASHANTI KUWAFUNIKA MADA MAUGO NA RASHIDI MATUMLA JUMAPILI P.T.A SABASABAA


Kocha msaidizi wa timu ya ngumi ya Ashanti. Fadhiri Gaston (kulia) akimwelekeza Iddy Ramadhani jinsi ya kupiga ngumi wakati wa mazoezi yake kabla ya kucheza mechi ya kirafiki jumapili hii katika ukumbi wa PTA sabasaba kushoto ni mchezaji Ramadhani Kimangare
Mabondia wa timu ya Ashanti Juma Fundi (kushoto) na Josephe Richard wakijifua katika ufukwe wa gymkhana Dar es salaam jana kwa ajiri ya maandalizi ya mapambano yao yatakayofanyika jumapili katika ukumbi wa P.T.A sabasaba



Mabondia wa Ashati kuwafunika Matumla, Maugo


Na Mwandishi wetu
MABONDIA Joseph Richard na Idd Ramadhani (Kg 54) wa klabu ya ngumi ya Ashanti watashindikiza pambano la ngumi la uzani wa Middle Weight kati ya Bondia Rashid Matumla 'Snake man' na Mada maugo litakalofanyika Julai 18 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es salaam jana, Kocha wa Ashanti Rajabu Mhamila 'Super D' alisema katika pambano hilo la Kg 75 mabondia hao kila mmoja atacheza pambano la kirafiki kusindikiza pambano hilo.

Alisema bondia Joseph Richard atacheza na bondia Kijepa Omari katika pambano la kilogramu 54 raundi 4 wakati bondia Iddi Ramadhani atacheza na Antony Matias katika mapambano hayo ya utangulizi ambayo yanatarajiwa kuwa na upinzani mkali tunataka kuwahakikishia kuwa vijana wa jiji Ashanti tumeiva kila idara.

"Mabondia wangu wawili ambao wanakuja juu katika mchezo wa ngumi hivi sasa watasindikiza pambano la Matumla na Maugo, hii ni nafasi pekee ambayo klabu yetu inajivunia nafasi hii," alisema Super D.
Kocha huyo alisema mabondia ameanza kuwanoa kwa ajili ya pambano hilo ambalo kubwa na kuongeza kuwa ana imani wataibuka na ushindi katika michezo watakayocheza katika wakati huu wanapojiandaa kuwa mabondia tishio.

Mbali na hilo kocha huyo alisema ili kuhakikisha viwango vya mabondia wake vinakua kila kukicha ameanzisha programu maalumu ya kujipima kila mwezi ili kuwaandalia mazingira ya kujiamini katika michuano mbalimbali watakaopata kushiriki katika michuano yao ya ndondi.

No comments:

Post a Comment