Friday, July 9, 2010
FRANCIS KIFUKWE ATANGAZA KULETA MAENDELEO KWA KIPINDI CHA MIEZI 6 TU
Francis Kifukwe
Francis Kifukwe akizungumza na waandishi wa habari kuusu makakati yake ya kuleta sakos yanga na maendeleo kwa kipindi cha miezi 6 tu endapo wana yanga watampa nafasi kuingia madarakani
MGOMBEA nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Francis Kifukwe anapewa nafasi kubwa ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Julai 18, mwaka huu.
Uchaguzi mkuu wa klabu hiyo umepangwa kufanyika katika ukumbi wa PTA uliopo kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wachama wa klabu hiyo Mohamed Sadiq Muddy Kala, alisema kuwa, Kifukwe ana nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kutokana na kuwa na uzoefu wa uongozi katika klabu hiyo.
“Huyo jamaa pamoja na mapungufu yake, bado ana nafasi ya kuwa Mwenyekiti wetu, uzoefu wake na mikakati aliyonayo, inatupa imani wana Yanga,” amesema.
Mwanachama huyo amesema hivi sasa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga, anaendelea na mipango yake ya kumsajili mchezaji nyota ambaye mambo yakikamilika, atatangazwa.
Wagombea wanaowania nafasi ya uenyekiti ni Kifukwe, Abeid Abeid, Lloyd Nchunga, Mbaraka Igangula na Edgar Chibura.
Nafasi ya makamu mwenyekiti inagombewa na Costantine Maligo, Ayoub Nyenza na Davis Mosha wakati nafasi za ujumbe wa Kamati ya Utendaji zinawaniwa na wanachama 29.
“Kifukwe baada ya kurejeshwa kwenye mbio za uchaguzi na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sasa njia ni nyeupe kwake,” amesema.
Awali, Kifukwe na Abeid waliondolewa katika mbio za uchaguzi wa klabu hiyo na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo baada ya kushindwa kuwasilisha vielelezo vilivyokuwa vikitakiwa, lakini Kamati ya TFF iliwarejesha kufuatia rufani yao.
Mgombea nafasi ya uwenyekiti wa Yanga Francis Kifukwe (kushoto) akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa kumwaga sela zake leo
No comments:
Post a Comment