Friday, July 9, 2010

ZANTEL NA TIGO ZAJIUNGA NA NMB MOBILE


BENK ya NMB imeungana na Kampuni ya simu za mkononi Zantel na Tigo kwenye huduma ya NMB Mobile ili kuwapa nafasi wateja wa NMB kutumia huduma hiyo kupitia mitandao hiyo.

Hadi sasa idadi ya mitandaa ambayo imeunganoshwa na huduma hiyo ya NMB Mobile imefikia minne ambapo mbali na Zantel na Tigo pia huduma hiyo ilikuwa ikitolewa na NMB kwa wateja waliokuwa wanatumia mtandao wa Vodacom na Zain.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya NMB Mobile kwenye mtandao wa Zantel na Tigo Mkurugenzi wa NMB Bw. Ben Christiaanse alisema hadi sasa huduma ya NMB Mobile imetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ikiwa inatumia mitandao ya Zain na Vodacom.

"NMB Mobile inatimiza kwaka mmoja sasa ikiwa na jumla ya wateja 250,000 wakati tukiwa tumeungana na wateja wanaotumia mtandao wa Vodacom na Zain lakini sasa tumeongeza mitandao mingine miwili ambayo ni Zantel na Tigo ili kuwapa fursa wateja wetu wanaotumia mitandao yote kupata huduma ya NMB Mobile,"alisema Bw. Christiaanse.

Alisema kwa wateja wa huduma hiyo ambao bado hawajajiunga na NMB Mobile watatakiwa kujiunga kwa kuandika alama ya nyota kisha 150 nyota 66 nyota 123 halafu alama ya reli ambapo moja kwa moja atakuwa ameungwa katika huduma hiyo.

Alisema huduma ya NMB Mobile inamuwezesha mteja kutuma fedha, kuangalia salio, kununua luku, kununua muda wa hewani wa Zantel, Tigo, Vodacom na Zain.

Alisema pia mteja anaweza kujiunga na huduma ya NMB Mobile kwa kutumia mashine za kutolea fedha ATM ambapo kwa sasa Benki hiyo inamashinne zaidi ya 300 na kwamba hadi mwishoni mwa mwaka huu wanatarajia kuwa na ATM 380.

No comments:

Post a Comment