Marquee
tangazo
Wednesday, September 8, 2010
FM ACADEMIA KUZINDUA ALBAM SIKU YA IDDI
Mwanamziki mpya wa bendi ya FM academia, Hafsa Kazinja,(kushoto) akiimba mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana wakati wa utambulisho wa uzinduzi wa albam mpya ya vuta nikufute itakayozinduliwa siku ya Iddi mosi katikati ni rais wa bendi hiyo Nyoshi el Sadaat na Ofisa Mahusiano wa Kampuni ya Zain Muganyizi Mutta ambao ni wazamini
BENDI ya Muziki wa dansi ya FM Academia 'Ngwasuma' inatarajia kumtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja aliyejiunga na bendi hiyo hivi karibuni.
Utambulisho huo utaenda sambamba na uzinduzi wa albamu ya sita ya bendi hiyo ya Vuta ni Kuvute unaotarajia kufanyika sikukuu ya Idd mosi katika ukumbi wa Diaomd Jubilee, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Rais wa bendi hiyo Nyoshi el Saadat alisema, mwanamuziki huyo ameshiriki kuimba katika baadhi ya nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ambapo katika uzinduzi huo atatambulishwa rasmi pamoja na wanamuziki wengine wanne kutokea Kongo (DRC) waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni.
Alisema, wanamuziki hao pia wameshiriki kwa kiasi kikubwa katika kuimba nyimbo za albamu hiyo ambapo mashabiki wakae tayari kusikia sauti mpya katika albamu hiyo ikiwa ni pamoja na za wanamuziki wakongwe wa bendi hiyo.
"Tutamtambulisha Hafsa ikiwa ni pamoja na wanamuziki wengine wanne waliojiunga na bendi hii hivi karibuni na wameshiriki katika kuimba baadhi ya nyimbo zilizopo katika albamu yetu hii mpya," alisema Nyoshi.
Aliwataja wanamuziki hao watakaotambulishwa sambamba na Hafsa kuwa ni Kamanyola, Ngronii, Sosoliso na Chekeda ambapo baadhi yao ni waimbaji na wapiga vyombo.
Alizitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo kuwa ni Vuta ni Kuvute, Heshima kwa Wanawake, Mwili wangu, Angalia shida yangu, Fadhila kwa mama, Usiku wa Jumatano, Mgeni, Jasmin, Intro Ngwasuma Mathematics Mayemba, Heineken Ngwasuma na Moses Katumbi.
Alisema, pamoja na kutambulisha nyimbo hizo pia zitapambwa na mitindo mipya ambayo wataitambulisha rasmi siku hiyo ingwa imeishaanza kusikika kama Pikipiki, Mayemba na Utamu wa Vanila.
Nyoshi alisema wadhamini katika uzinduzi huo ni Henken ambao pia watazindua bia ya Henken mpya iliyokatika ujazo mdogo ambayo mtumiaji hatahitajika kurudisha chupa pindi ainunuapo wakiwa pamoja na mtandao wa simu wa Zain ambao umedhamini kisi cha fedha zaidi ya sh. Milioni 15 kwa ajili ya uzinduzi huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment