Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 9, 2010

ZAIN YAFUTURISHA WATOTO YATIMA


Zain yawapa raha yatima wa Dar es Salaam

Kampuni ya simu za mkononi ya Zain kupitia mradi wake wa Build Our Nation, juzi ilifuturisha watoto yatima kutoka vituo vitatu vya kusaidia watoto yatima vilivyoko Dar es Salaam.

Vituo vilivyofuturishwa ni Madrassat cha Magomeni, Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Mbagala na Umra Orphanage cha Magomeni. Jumla ya watoto 320 kutoka katika vituo hivyo walifaidika na futari hiyo.

Mbali na futari Zain pia ilitoa misaada ya vyakula kama vile mafuta ya kupikia, unga, mchele, sabuni za kufuria vyenye thamani milioni saba.

Akiongea wakati wa hafla hiyo Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tunu Kavishe alisema kuwa Zain wameamua kutoa msaada huo kama sehemu yake ya kujali jamii kupitia mradi wake wa Build Our Nation.

“Zain ni kampuni ambayo ina mkakati wa kusaidia jamii, na ndiyo mana leo tumeamua kufuturu na watoto yatima kutoka katika vituo vitatu vya hapa Dar es Salaam, huu ni utaratibu ambao tutauendeleza na tumekuwa tukiufanya kila mara,” alisema

Akizungumzia msaada huo, Mwakilishi wa Bakwata ambaye aliongea kwa niaba ya vituo vilivyopata misaada hiyo, Mohamed Khamis alisema kuwa wao wamefarijika na jinsi Zain ilivyoamua kutoa misaada hiyo.

“Tunawashukuru sana Zain kwa kuwakumbuka watoto hawa yatima katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na naomba msaada huu uwe endelevu ili watoto hawa nao wapate fursa ya kufurahia maisha yao”. .

Kavishe alisema kuwa zaidi ya miaka mitano, mbali na juhudi za kusaidia jamii kwa namna mbalimbali hapa nchini, hususan katika sekta ya elimu, kampuni ya simu ya Zain imejiwekea utaratibu wa kuwa inafuturisha wadau mbalimbali katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mikoa mingine ambayo hapa awali ilifaidika na utaratibu huu wakati wa mfungo wa mwezi wa ramadhani kwa mwaka huu ni Pemba, Songea, na Mbeya, Morogoro, Tabora, Kigoma, Kagera na Tanga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...