Friday, November 26, 2010

MAONESHO YA BADHAA ZA MIKONO YAZINDULIWA COCO BEACH LEO


Sisi wanachama wa TanCraft na NASME/WEEC tunayofuraha sana kwa siku hii ya leo kwa kuitikia mwaliko wetu kujumuika nasi ili kufanikisha tukio la leo la ufunguzi wa maonyesho ya 5 ya kazi za mikono. Mheshimiwa Katibu Mkuu

Katika maonyesho haya tunao wanaonyeshaji toka Tanzania ----Malawi --- na Kenya ---- katika sekta zifuatazo:







1. Vikapu

2. Ufinyazi

3.Bidhaa za Ngozi

4. Uchongaji wa Vinyago

5. Nguo na Ushonaji

6. Uchoraji na Picha

7. Usindikaji wa Vyakula

8. Watoa huduma mbalimali


Kauli mbiu yetu ni

NJOO, ANGALIA NA NUNUA BIDHAA ZA ZILIZOTENGENEZWA TANZANIA NA MALAWI.


  1. UTANGULIZI:

Trade Facilitation Office (TFOC) ya Canada wakishirikiana na Bodi ya Biashara ya Nje (BET) pamoja na Shirikia la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) waliandaa na kuratibu tukio la uendelezaji wa masoko ya kazi za mikono hapa Tanzania. Bidhaa ziliandaliwa na maonyesho ya kazi za mikono yalifanyika katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba mwezi April 2006 na yalifunguliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa wakati huo

Wakati huo ndipo (TanCraft) ikaanzishwa mwezi April 2006. Shughuli za usajili rasmi kisheria zilifanyika mnamo Mwezi August 2006 chama kilipata Cheti cha usajili no.SO. 14470 kilichotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  1. KAZI ILIYOFANYIKA:

Mheshimiwa Katibu Mkuu


Katika majukumu ambayo tuliyapa kipaumbele ni:

  1. Kuandaa Kitabu cha orodha ya wazalishaji wa kazi za mikono hapa Tanzania kwa kusaidiana Trade Facilitation Office of Canada 2007

  2. Kuandaa maonyesho ya Kwanza ya TanCraft ambayo yalifanyika katika Viwanja vya Karimjee 2007

  3. Kuandaa Maonyesho ya Pili yaliofanyika nchini Malawi mwaka 2008 kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi

  4. Kuandaa maonyesho ya Tatu yaliofanyika tena nchini Malawi kwa kushirikiana na NASME chama ambacho kinashughulika na wajasiriamali wadogo nchini pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi 2009

  5. Kuanda semina mbalimbali zinazohusu ujasiriamali 2009, 2010

  6. Kuandaa maonyesho mengine makubwa nchini Malawi kwa kushirikiana na wenzetu NASME/WEEC ya Malawi mjini Lilongwe kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi enzi za Mh. Balozi Mstaafu Rashid Makame.

  7. Kuandaa semina mbalimbali za kuimarisha wanachama kwenye biashara zao ili waweze kuongeza tija na pia kiwango cha uzalishaji bidhaa bora.

  8. Kuandaa semina za Ukimwi mahali biashara na kazi.


1.1 MALENGO YA CHAMA:

1.1.1 Kuendeleza sekta ya kazi za mikono kwa kuhamasisha miradi mbalimbali yenye lengo la kuunganisha sekta nzima na kutumia raslimali, ujuzi na utaalamu mbali mbali uliopo katika sekta ya kazi za mikono na sekta zinazohusiana;


1.1.2 Kutambua matatizo yaliyomo katika sekta ya kazi za mikono ambayo yanazuia kukua kwa sekta na kushiriki katika kutatua.


      1. Kuwasaidia wanachama wake ili waweze kupata misaada inayohitajiwa kwa ajili ya masoko ya nje ya nchi pamoja na upatikanaji wa mali ghafi


      1. Kuandaa mazingira na kujenga uwezo wa kubadilishana taarifa na uzoefu kati ya wazalishaji wa kazi za mikono pamoja na wafanyabiashara wa sekta ya kazi za mikono kwa upande mmoja na kushirikiana na mashiriki ya serikali ili kupata matokeo mazuri katika matumizi ya rasilimali zilizopo pasipo kusababisha uharibifu wa mazingira;


      1. Kushirikiana na mashirika ya hapa nchini na ya kimataifa katika kuhamasisha biashara kati ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea ili kupata msaada na ushirikiano ambao utaleta manufaa kwa chama na wanachama wake.


  1. CHANGAMOTO, MAHITAJI NA MAPENDEKEZO:

  1. Eneo/sehemu ya pamoja ya kuendeshea shughuli zetu za kila siku ; Kwa vile TanCraft ni asasi inayounganisha Watanzania wote; imethibitika kuwa na wasanii ni wengi kiasi cha kulazimika kuwa na eneo maalum la kuuzia na hata kuzalishia

TANCRAFT inaomba ipewe jengo au sehemu katika mikoa inayotembelewa na watalii wengi kama vile Arusha,na DSM kule TRIDO. Hili ltaisaidia sana Tancraft kwani tukiwa na eneo moja la uzalishaji tutakuwa na ubora wa hali ya juu na unaofanana kwa ajili ya soko kubwa na hilo litaongeza kipato kwa wasanii na kuongeza ajira.


  1. Mhe. Katibu Mkuu

TanCraft kwa kuona kuwa kuna haja ya kushirikiana na nchi za Jirani kama Malawi tuliamua kwenye Maonyesho yaliopita kule Lilongwe kwamba kila mwaka mara moja maonyesho yatafanyika katika nchi ya Tanzania naMalawi, ndio maana leo hii tuko na wajasiriamali kutoka Malawi kutimiza makubaliano yetu.

Tumealika wenzetu kutoka Kenya ili tuweze kuwa nao pamoja katika soko hili la Kusini mwa Afrika ambapo baadae tunataka kuwashirikisha Zambia, Botswana na Zimbambwe tuwe pamoja katika kuondoa umaskini katika jamii yetu.


  1. MIPANGO YA BAADAYE:

  • Kuziwezesha na kuziboresha bidhaa za sanaa za mikono Tanzania

  • Kufanya kazi kwa karibu zaidi na serikali yetu ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa na chuo maalumu cha ufundishaji na udumishaji wa sanaa za mikono .


  1. Kujenga nafasi kati ya wazalishaji wa kazi za mikono ili wajue umuhimu na nguvu ya kuwa na huduma za masoko ambazo ni endelevu.


8. Wenye kutoa huduma mablimbali


  1. SHUKURANI:

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wafuatao ambao wamesaidia mno kuifikisha TanCraft hapa ilipo leo.

  1. Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko,

Wizara imekuwa ikiwateua maofisa wao kutusaidia katika maandalizi na pia hata kufuatana nasi katika maonyesho huko Malawi ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa kiwango cha Juu.


  1. Ubalozi wa Tanzania kule Malawi, Ubalozi wetu umekuwa ukituunganisha na serikali ya Malawi na Wajasiriamali kila tunapohitaji msaada wao ingekuwa ni vigumu sana kama wasingeonyesha juhudi hii kuanzia mwanzo hasa mwaka 2008 hadi leo 2010

  2. Ubalozi wa Malawi nchini Tanzania kwa kushirikiana nasi katika maandalizi ya aina zote na pia kuwa kiungo kikubwa cha mawasiliano kati yetu na wenzetu wa Malawi.

  3. Wafadhili wetu hapa Tanzania Matching Grant Program chini ya ( TPSF) kwa kuwawezesha wajasiriamali kushiriki maonyeshomabalimbali semina,utafit wabidhaa hapa ndani ya nchi na nje wa masoko,kujiendeleza katika somo la kiingereza nk.

  4. Mmiliki wa CoCo Beach kwa kutupa eneo la kuonyeshea biashara zetu kwa na pia kushirikiana nasi katika maandalizi yote bila kuchoka.

  5. Jeshi la Polisi Mkoa wa DSMi kwa kushirikiana nasi katika kuhakikisha Usalama wa Raia na mali zao

  1. Tunapenda kuwashukuru wote waliotusaidia kwa namna moja au nyingine ili kufanikisha kazi hii na kukiweka chama hapa kilipo hasa wajasiriamali wenyewe kwa kujitoa kuonyesha bidhaa zao kila wanapohitajika, kuhudhuria semina zote zilizoandaliwa na chama na pia

kuchangia gharama zilizotakiwa, na viongozi wenzangu wote kwa kujitoa muda wao na kushiriki katika mikutano yote bila kuchoka.

Mheshimiwa Katibu Mkuu

Tunakukaribisha uweze kusema na Wajasiriamali

KARIBU MHESHIMIWA KATIBU MKUU

No comments:

Post a Comment