Friday, May 27, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 6 WA KIMATAIFA WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijaribu kuvaa miwani ili kuweza kuona picha iliyokuwa ikionyeshwa ukutani kupitia Screen na Projector (Animation Fils) , wakati alipotembelea Banda la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Elimu na Mafunzo, Shukuru Kawambwa (kulia) ni Mkurugenzi wa Designmate Animation Films, Colonel Basavaraj
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Imelda Lutebinga na Langton Chibura wakati alipotembelea Banda lao la maonyesho la SEACOM Tanzania Ltd.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, baada ya kufungua mkutano.

Emaanuel ambaye ni mtanzania pekee aliyeshiriki katika mkutano huo kupresent Paper.

Waziri wa Elimu wa na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, akizungumza baada ya makamu wa rais kufungua mkutano huo.


Baadhi ya Mawaziri na Manaibu wao waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo, wakifuatilia maonyesho ya picha zilizokuwa zikionyeshwa katika Screen za ukutani.


Picha ya pamoja na baadhi ya watu waliopresent paper zao.

No comments:

Post a Comment