Friday, May 27, 2011

MKE WA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MAMA ASHA BILAL, AZINDUA MFUKO WA PAMOJA TUSHIKAMANE WA KUSAIDIA WAZEE WASIOJIWEZA

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza wakati akisoma hotuba yake ya uzinduzi rasmi wa Mfuko wa kusaidia Wazee wasiojiweza wa ‘Pamoja Tushikamane’ ulio chini ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tushikamane Pamoja Faundation. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mama Asha Bilal (kushoto) akiongozana na Mwenyekiti wa mfuko huo kuingia ukumbini baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya New Africa.

Mtunza hazina wa mfuko huo (kulia) akionyesha kidani cha Silver alichonunua kwa Sh. 750,000 baada ya kupigwa mnada, ambacho thamani yake halisi ilikuwa ni Sh. 150,000.
Mmoja kati ya wageni waalikwa, Bi. Eshe Sururu, akizungumza kutangaza kiasi alichotoa kuchangia mfuko huo jana, ambapo alitangaza kuchangia Sh. 500.000.

Mmoja kati ya wafanyakazi wa mfuko huo akibofya kitufye cha Kompyuta kuonyesha baadhi ya picha za watu waliofanikiwa kuwatembelea.

Baadhi ya wageni walioalikwa kuhudhuria hafla hiyo.

Baadhi ya wageni waalikwa.

Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wanaojitolea kufanya kazi katika mfuko huo wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa.........

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza jambo na Balozi Juma Mwapachu, baada ya kuzindua rasmi mfuko wa Tushikamane Pamoja Faundation, iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa.

No comments:

Post a Comment