Sunday, June 26, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MADAWA YA KULEVYA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha kutumia madawa hayo. Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa.



Muelimisha Rika kutoka Banda la Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Catherine Saoke, akifafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Msingi, Kilimahewa ya Temeke, Mubaraka Abdallah na Ally Kionda, kuhusu utofauti na madhara kati ya dawa ya Cocaine na Heroin, wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda hilo kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa katika moja ya mabanda hayo kwa ajili ya maonyesho.


Vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya, Rajab Huseein na Tatu Mapando, wakitoa ushuhuda kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kuacha kutumia madawa hayo.

No comments:

Post a Comment