Wednesday, July 6, 2011

Umeionja? Umeinywa? Ni Dodoma Wine, Ni Imagi Ndani ya Jengo La Tanzania Distilleries Ltd, Sabasaba

















Mratibu wa Masoko ya Nje Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL), Bavon Ndumbati, akionesha Mvinyo mpya wa Imagi unachotengenezwa na kampuni hiyo,leo mchana katika Jengo la Konyagi kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya Kimataifa ya Biasahra (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Tanzania Distilleries Ltd (TDL), hivi karibuni walitambulisha aina mbili za Mvinyo, Dodoma Wine na Imagi ambazo zimetokea kupendwa sana na wanywaji kutokana na ladha yake nzuri na ya kusisimua. Katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara Mvinyo huo unapatikana kwa wingi kwenye Jengo la Konyagi.







Mratibu wa Masoko ya Nje wa Tanzania Distilleries Ltd (TDL), akimuonesha mmoja ya wananchi waliotembela Jengo la Konyagi aina mpya ya Mvinyo wa Dododma (Dodoma Wine)







Wadau wakiwa na Mvinyo wa Dodoma Wine na Imagi ndani ya Jengo la Tanzania Distilleries Ltd (TDL), leo mchana, katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).







Da' 'Nanihii' akijichukulia Mvinyo wa Dodoma na Imagi ndani ya Jengo la Tanzania Distilleries Ltd (TDL) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba leo mchana.







Kazi kwako, hapo utapata Mvinyo wa Dodoma na Imagi kwa kiasi utakacho. Ni ndani ya Jengo la Tanzania Distilleries Ltd (TDL), katika Maonesho ya Kimataifa ya Baishara (Sabasaba). Pia utaelekezwa aina mbali mbali za vileo vinavyotengenezwa na kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment