Muigiza Steven Kanumba akimkabidhi msaada wa chakula mtoto Rukia Yazidu kwa niaba ya wenzake wakati Kampuni ya Steps entertainment na Kanumba the great films zilipotoa msaada wa vifaa mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dar es salaam leo.
Steven Kanumba na Afisa uhusiano na Jamiii wa Stepe Selles Mapunda wakionyesha moja ya kipeperushi kinacoelezea filamu ya Devl's Kingdom katika kituo cha kula watoto yatima cha CHAKUWAMA Sinza.
Kampuni ya Steps entertainment na Kanumba the great films kwa pamoja, leo hii inasherehesha tukio la kihistoria katika tasnia ya filamu Tanzania. Tukio lenyewe ni kuhusu utolewaji wa filamu ya kwanza iliyoigizwa kwa ushirikiano kati ya wasanii nguli barani Afrika. Ramsey Tonkubo Nouah wa Nigeria na Steven Kanumba wa Tanzania wameshirikiana na kufanya filamu bomba iitwayo “Devil’s Kingdom” ambayo itakuwa sokoni kesho ijumaa nchi nzima. “Jamani hatuko hapa kusherehekea hilo tu, bali tuko hapa pia kuwapa hamasa wasanii wengine hapa nchini hasa wachanga (Under-ground) kwamba Steps imejizatiti katika kuinua vipaji vya wasanii wachanga na aliyepewa jukumu la kuongoza filamu za Steps zitakazoshirikisha wasanii wapya kila mwezi ni mwongozaji wa filamu Selles Mapunda ambaye amepangiwa kutengeneza filamu 12 kuanzia leo mpaka mwezi kama huu mwakani akishirikisha pia na wasanii nguli hapa nchini akiwemo Steven Kanumba, Ray, JB na wengineo”. Alisema hayo Selles Mapunda ambaye pia ni Afisa Mahusiano ya Jamii katika kampuni ya Steps Entertainment. (Community Relation Officer). Amesema huu ni mwanzo wa safari ya Steps kuhakikisha kwamba Tasnia ya filamu Tanzania inakua kimataifa, il-hali mafanikio yake yanasaidia pia jamii na hasa wasiojiweza na watoto. “Mungu aibariki hii tasnia” hayo pia ni moja ya maneno ya mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Steps Jairaj Domodoran. Bw. Selles Mapunda ameyasema hayo wakati kampuni hiyo ikishirikiana na Kanumba The Great wakati wote kwa pamoja walipotoa msaadwa wa vifaa mbalimbali katika kitua cha kulelea watoto cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dar es salaam ambapo walitoa msaada wa Chakula , Mchele, Sabuni, Nguo na vitu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment