Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 21, 2011

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema milango iko wazi kwa wawekeza wa China


NA MWANDISHI BEIJING

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema milango iko wazi kwa wawekeza wa China kuja nchini kuwekeza ikiwa ni hatua itakayosaidia kuinua uchumi na maendeleo kwa ujumla.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame alieleza hayo alipokutana na uongozi wa kampuni ya Beijing Construction Engenearing Group ya China.

Dk. Mwinyihaji aliongoza wajumbe wa warsha ya watendaji wa SMZ walioko China kujifunza mbinu za kuyatumia maeneo tengefu ya uchumi, mkutano uliofanyika Mako Makuu ya Kampuni hiyo mjini Beijing.

Mwinyihaji ambaye ni Waziri wa Nchi na Ofisi ya Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alisema milango ya uwekezaji Zanzibar iko wazi na kuikaribisha nchi hiyo kuja kuwekeza hali itakayosaidia kukuza uchumi wa Visiwa hiyo.

Waziri Mwinyihaji alisema China na Zanzibar zimekuwa na urafiki na uhusiano wa muda mrefu ambapo nchi hiyo imekuwa ikipata misaada mbali mbali Zanzibar ikiwemo ujenzi wa Jengo la abiria katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume kazi ambayo inatarajiwa kumaliza mwaka 2013

Alisema Zanzibar inahitaji mabadiliko makubwa katika Nyanja za uchumi na miundombinu ya majengo ya ofisi na kuimarisha makazi ya wananchi wake, ili kuweza kutumia eneo dogo la ardhi ambalo linahitajika kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kilimo.

Dk. Mwinyihaji aliridhishwa na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na Kampuni hiyo ambayo yalithibitishwa baada ya kutembelea katika eneo linalojengwa nyuma 16 za ghorofa kusini mwa Beijing ambazo ni kwa ajili ya makazi ya wananchi na ofisi mbalimblai za serikalina, taasisi binafsi zitakazoweza kuwahudumia wananchi wa huko.

Alieleza dhamira ya ziara hiyo iliyoandaliwa na serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwaleta watendaji wake kuja kujifunza maendeleo ya haraka ya ukuaji wa kiuchumi yaliyofikiwa nchini China ili Zanzibar nayo kupata nafasi ya kuimarisha uchumi wake kupitia katika maeneo tengefu ya uchumi ikiwemo Micheweni, viwanda vidogo vidogo vya Amani na Fumba ambayo yalitengwa kwa kazi hiyo.

Aidha alisisitiza ujenzi wa jengo la abiria la Uwanja wa ndege limazike kwa wakati ili kuongeza kasi ya Zanzibar kuwa kitovu cha biashara katika usafirishaji wa mizigo na abiria, sambamba na kuongeza idadi ya watalii ambayo ni ndiyo sekta moja wapo inayoingizia fedha nyingi za kigeni

Kwa upande wake Makamo wa Rais wa Kampuni ya Beijing Construction Engenearing Group Yang Qing aliahidi ujenzi huo utamalizika kwa wakati uliowekwa ili uweze kutoa huduma kwa wananchi na wageni

Alisema kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma za ujenzi wa majengo ya Ofisi za serikali za Kibalozi na hoteli za kitalii ndani na nje ya China ikiwemo nchi za Ulaya Asia na Bara la Afrika na Tanzania ambapo ujenzi wa uwanja wa Taifa wa mpira jijini Dar es Salaa ulojengwa na kampuni hiyo

Mapema ujumbe huo ulitembelea katika uwanja wa michezo uliotumika katika mashindano ya Olimpik katika mwaka 2008 yaliyofanyika nchini humo.

habari kwa msaada wa http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...