Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 25, 2011

TIGO YATOA MSAADA WA VITABU KWA SHULE YA MSINGI TOANGOMA


Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo kwa kupitia kampeni yake ya “Tigo tuChange” imetoa msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule ya msingi Tuangoma iliyopo manispaa ya temeke ikiwa ni moja kati ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na kampuni hii katika kuchangia sekta ya elimu ili kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.

Shule ya msingi Toangoma ya jijini DSM ni moja kati ya shule za msingi mbalimbali nchini zitakazofaidika na kampeni hii ya “Tigo tuChange” ambapo hivi karibuni vitabu vitasambazwa katika mikoa ya Tabora, Kagera na Mtwara.
Akielezea madhumuni ya kampeni ya Tigo Tuchange wakati wa kukabidhi vitabu katika shule hiyo, mwanasheria wa kampuni ya MIC – TIGO TUMAINI SEKWA SHIJA amesema Tigo kwa namna ya pekee imeguswa na matatizo yanayozikumba shule mbalimbali za msing na yamekuwa kikwazo kikubwa katika kuongeza kiwango cha elimu nchini ndio maana baada ya kutoa vibao vya mapajani kwa wingi katika shule mbalimbali sasa ni ni vitabu.

SHIJA ameongeza kuwa uzalendo wa watanzania na hasa katika kuipenda tigo umetoa msukumo wa wao kurudisha sehemu ya faida kwa jamii, ‘watanzania wameendelea kuwa msaada mkubwa kwetu na wameendelea kutuunga mkono siku zote sasa na sisi kwanamna ya pekee hasa ukizingatia kuwa Tigo ni sehemu ya watanzania hatuna budi kurudisha sehemu ya kile tunachokipata kwa jamii inayotuunga mkono siku zote.’
Naye mkurugenzi wa Mamlaka ya elimu Tanzania ROSEMARY LULABUKA amesema anafurahia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia sekta ya elimu. ‘Hatua hii ni nzuri na yenye manufaa kwa Taifa kwani vitabu vimeendelea kuwa tatizo kubwa katika sehemu mbalmbali ndani ya nchi na hivyo tunaishukuru tigo kwa kutufuata na kutaka ushiriki wetu katika kampeni hii na tungependa mashirika na taasisi binafsi na za serikali kuiga mfano huu wa Tigo katika kuchangia elimu ili tuweze kuhakikisha watoto wanapata nyezo muhimu za kujifunzia wakiwa shuleni”

SHIJA amesema kuwa jumla ya shilingi 25,930,160 zilipatikana katika program maalum ya Tigo Tuchange iliyofanyika tarehe 9 mwezi wa saba 2011 kuanzia saa tatu mpaka saa nne asubuhi ambapo ndani ya muda huo mteja yeyote wa Tigo aliyenunua muda wa maongezi wa kuanzia shilingi mia tano na kuendelea alichangia kupatikana kwa fedha hizo ambazo ndizo zimetumka katika kununulia vitabu hivyo ambavyo vitatolewa kwa shule za msingi kwa kupitia mwongozo unaotolewa na mamlaka ya elimu Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...