Friday, November 18, 2011

MFALME MSWATI AKOMALIWA NA VIONGOZI WA DINI ATOKE MADARAKANI





Mfalme Mswati wa Swaziland.


Mabinti wa Kiswaziland wakiwa wamevalia mavazi ya kikabila wakati wa sherehe za kupita mbele ya Mfalme Mswati ili achague Mke mwingine wa kuoa kama mila zao zinavyotaka.


Askofu Meshack Mabuza.

Wakati vugu vugu linaloendelea katika Mataifa mbali mbali ndani ya Bara la Africa, la wananchi kuwatoa watawala ambao wamekaa muda mrefu katika madaraka yao, sasa laamia Swaziland kwa Mfalme Mswati.

Hali hiyo imepelekea mpaka viongozi wa dini kuingilia kati kwa kuitaka serikali ya Mswati iweze kutoka madarakani na kuitisha uchaguzi ambao utakuwa wa kidemokrasia wa vyama vingi.

Hayo yametokea kutokana na utawala wa Mswati kushindwa kuwalipa mishahara baadhi ya wafanyakazi wa Serikali kwa wakati husika na kuwaomba wasubiri mpaka mwezi wa Disemba na mambo mengine mengi ambayo yanatokea Nchini Swaziland.

Hali hiyo pia imetokana na wananchi kuulalamikia utawala wake kuwa ni wa kifisadi na kuifanya serikali yake kushindwa kufanya sherehe ya kuadhimisha miaka 25 ya utawala wake.

No comments:

Post a Comment