Friday, November 18, 2011

UKOO WA CHADEMA BUNGENI WAANIKWA: GAZETI LA UHURU






BAADHI ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.


"Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa Mwenyekiti wa Chama ana ndugu watatu, Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme? Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, Samahani Mh. Ndesamburo"

Akichangia juzi, muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011,
Assumpter Mshama (Nkenge –CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA.

“Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi,” alihoji.

Aliongeza: “Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo.

“CCM ilitengeneza utaratibu wa kupata viongozi wa viti maalumu, wao si kifalme tu, tuseme ni kaskazini tu, nawashangaa watu wanaojiita CHADEMA, wenzako wako bungeni huulizi wamepatikanaje.”

Kwa upande wake, Livingstone Lusinde
(Mtera-CCM), akichangia jana, alisema CHADEMA ndiyo yenye tabia ya kupeana madaraka kwa kufuata unasaba.

Alisema viti maalumu vimetolewa kwa unasaba, na kama hilo lingefanywa na CCM ingekuwa wimbo kila siku.

“Ndiyo maana humu ndani wamo wakwe, dada, kaka, ingekuwa ni kwa CCM ingekuwa wimbo kila siku. Nashangaa wanaposema rais anaongoza kifalme,” alisema.

Lusinde alisema wanaotoa vitisho vya kuandamana na kwamba wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba waachwe wafanye hivyo kwani wa kuzuia fujo wapo.

“Wanaotaka kufanya vurugu waachwe tu, wengine wanasema wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba. Mimi sipo tayari nataka nione katiba mpya, ambayo Watanzania wamekuwa wakiitaka kwa muda mrefu,” alisema.

Lusinde aliohoji busara ya wazee wa CHADEMA ambao wameshindwa kutoa kauli baada ya vijana wao kuchafua hali ya hewa.

Mbunge huyo alisema CHADEMA inafanya hivyo kutokana na ahadi ya fedha waliyopewa na Ujerumani.

CHADEMA imesusa kujadili muswada huo unaohitimishwa leo, baada ya kujadiliwa kwa siku nne, kwa kile wanachodai umekosa uhalali kwa kukiuka Kanuni za Bunge.

Hata hivyo, CHADEMA imekuwa ikijibu hoja zinazojadiliwa na wabunge bungeni, kupitia mikutano na waandishi wa habari inayofanyika kila siku mchana, ambapo katika mkutano wa jana imeliomba bunge kutopitisha muswada huo.

Mikutano hiyo imekuwa ikiitishwa na viongozi wa CHADEMA, John Mnyika (Ubungo) na Tundu Lissu (Singida Mashariki), ambaye Jumatatu wiki hii aliwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, kuhusu muswada huo.

Katika maoni hayo, alipendekeza baadhi ya mambo kwenye muswada huo na pia aliwachefua wabunge kutokana na hoja zake kuhusu Muungano na pia kutamka kuwa Tanzania ina urais wa kifalme.

John Lwanji (Manyoni Magharibi-CCM), alisema wanachofanya CHADEMA ni sawa na kiini macho katika mazingaombwe, akitumia neno abrakadebra.

Benardetha Mushashu (Viti Maalumu-CCM), alihoji CHADEMA walitoka bungeni kwa kanuni gani na mbona hawachukuliwi hatua.

“Wanawalaghai wananchi, Lissu alichangia muswada. Wanaharakati wanatangaza kufanya maandamano yasiyo na kikomo kama kwamba hakuna serikali, wakijaribu wataona,” alisema.

Alisema kinachoendelea Arusha ni matokeo ya maandamano ya kila siku, ambayo hivi sasa yameanza kushamiri Mwanza, ambapo watu wanapigwa mabomu ya machozi.

“Libya walianza na maandamano, Gaddafi ameuawa, lakini hivi sasa wanauana,” alisema.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema hamlazimishi mbunge kuingia kwenye kamati, bali anachofanya ni kufuata Kanuni za Bunge na Katiba.

Alisema hayo bungeni jana, kutokana na malalamiko yanayotolewa na CHADEMA na NCCR-Mageuzi kwamba, spika alilazimisha wabunge kuingia katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kujadili muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.

Spika Anne alisema CHADEMA hawakutumia busara kutoka ndani ya ukumbi wa bunge, bali wangewasilisha hoja zao, na endapo wangeshindwa, basi wangeshindwa kishujaa.















19 comments:

  1. HIVI CHADEMA BILA NDESAMBURO KITAENDA HUU NI MUHULA MWISHO WA NDESAMBURO AKIONDOKA UFADHILI WATAUPATA WAPI NI VEMA CHAMA KIKAWA NA MATAWI TANZANIA NZIMA KWA MANENO MENGINE KIWE CHA KITAIFA

    ReplyDelete
    Replies
    1. HATA IKIWA WOTE NI WATOTO WA BABA MMOJA TUNACHOANGALIA NI LENGO LAO NI KUTUFISADI AU KUTUTETEA,TUNAWASHUKURU SANA FAMILIA HIZO ZINAZOTUMIA RASILIMALI ZAO KUTETEA TAIFA ZIMA.. KULIKO HII BABA ANA NGUVU MWANA YUKO NJE ANACHOTA PESA NA KUFANYA KILA ANACHOTAKA NA HAGUSWI. NTATAJA ILI MSEME KAMA HAWANA NDUGU, HUSEIN MWINYI,JANUARY MAKAMBA,HAWA GHASIA,RIDHIWANI KIKWETE,NAPE NNAUYE,LIVINGSTONE LUSINDE,MAGRET SITTA,SAMWELI SITTA,JOHN MALECELA,ANA KILANGO,AISHA KIGODA,ABDALA KIGODA,BEATRICE SHELUKINDO,ZHAKIA MEGHJI AISEE NI WENGI SANA,.HAPO CJAENDA KUANGALIA UDINI NDANI YA MASHIRIKA KAMA NSSF(HUKO NDO BALAA)

      Delete
    2. acha upuuzi wako,mi mwenyewe ni mwanachama wa chadema lakini hilo la kila mtu kumuweka ndugu yake siliafiki kabisa iwe kwa chadema au ccm,ndo maana kumbe tunaambiwa chadema ni ya kaskazini nimeelewa ni kwanini,chamsingi viongozi wetu wachague watu kwa misingi ya uwezo wao na si undugu na urafiki kama inavyojionesha kwa sasa,nilitarajia hili litokee kwa ccm ambao twawaita mafisadi kumbe hata chama chetu kina uozo wa undugu na ukabila,hilo halikubaliki kwa mtu yeyote mwenye busara!

      Delete
  2. AISEE.CHADEMA hata km wangekuwa baba mmoja wote tutaendelea kuwaunga mkono kuliko kuwa na majambazi wa CCM wanaodalali nch yetu utadhan wanahama kesho.tumewachoka eny majambaz sugu(CCM).ona sasa mpaka mnanyosheana silaha.Sis tunataka raslimal zetu ziwanufaishe watz wote na si majambaz wa CCM pekee.Halafu hoja hapa si undugu ni uwezo na udhalendo bila kusahau uadilifu.Ndan ya CCM kuna watu wana mabilion ya kutosha je wamezipata wap?jibu ni wameiba raslimali za nchi.hata la rada limewaumbua na wakat kunaushahid wa kutosha.hata waingeleza wanatushangaa sn kwamba n watu wa aina gan.wao wanauchungu na tz kuliko viongoz majambaz wa CCM.mtu anaye tetea CCM naye ni jambaz na mumuogope sn.CCM niwakolon weus bora wale weupe.MUNGU IBARIKI TZ.

    ReplyDelete
  3. ACHA USHABIKI KWENYE MAMBO YA MSINGI WEWE. CHADEMA NI CHAMA, KAMPUNI AU NGO?. KAMA NI CHAMA HAIWEZEKANI KOO KADHAA ZIKAWA KWENYE NAFASI ZA MAAMUZI WENGINE WASINDIKIZAJI. KAMA iliVYO FEDHA ZA RADA HII NAYO KALI.

    USHAURI USIZIDISHE USHABIKI KWANI UTAKUWA KIPOFU KUONA BAADHI YA MAMBO HATA KAMA NI UOZO

    ReplyDelete
  4. WEWE UNAONGEA NINI NYANI WAKATI WOTE HAONI KUNDULE KWENYE CCM MBONA WOTE WAKO NA WAKE ZAO NA WATOTO WAO BANA MNAFIKIRI WATU HAWAONI UNAMWAMBIA MWENZAKO AACHE USHABIKI WAKATI ANAONGEA UKWELI KABISA ACHA UJINGA WW YAN NATAMANI NIKUONE NIKUPIGE MAKOFI CCM KILA MTU YUKO NAMTOTO WAKE EBU FUNGA BAKULI LAKO WW MJINGA KWELI CHADEMA CHADEMA NDO MNAONA CHAMA CHA KUKIONEA MBONA MSISEME NCCR MAGEUZ MBATIA YUKO NA DADA YAKE JAMANI KWA UFUPI HIYO MADA MTU KAWA NA DADA YAKE SIJUI MTOTO IYACHE MAANA HAKUNA ALIYEKAMILI

    ReplyDelete
  5. SASA WAKALE WAPI?

    ReplyDelete
  6. CCM Chama bwana, hata mseme nini! maendeleo tuliyopata mpaka sasa yanathibitisha hilo. Mwenye macho haambiwi tazama.

    ReplyDelete
  7. wote mnafanana akili mnabaki kugombana wageni wanachuma nchi yenu mna laana nyie watanzania.

    ReplyDelete
  8. wote mnafanana akili mnabaki kugombana wageni wanachuma nchi yenu mna laana nyie watanzania.

    ReplyDelete
  9. yaan hamna aliye bora bali tumwachie mungu ndo atutee na kutupatia viongozi aliowapaka mafuta mwenyewe na watakaongoza nchi kwaa aman na kwa maslah ya kila mtanzania.

    ReplyDelete
  10. Wapinzani yao ngumu kapatikana jembe la kazi.

    ReplyDelete
  11. CHADEMA kaeni chini mjipange upya kwa uchaguzi wa mwaka 2015,
    walau hata wabunge wegi basi kama ikulu itashinikana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. MTAKAPOKOSA UFUMBUZI WA MALUMBANO YENU NIITENI NIWASAIDIE. NAONA KAMA WOTE NI WATOTO WA JUZI JUZI TU!!!

      Mzee wa Busara

      Delete
  12. Mtakapokosa ufumbuzi wa malumbano yenu mniite niwasaidie. Naona ninyi ni watoto wa juzi juzi tu!!1

    ReplyDelete