Wednesday, December 14, 2011

BFT YAWEKA WAZI PROGRAM YA MASHINDANO YA OLIMPIKI


SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa Tanzania (BFT) linatarajia kuweka wazi programu yao ya kushiriki mashindano ya kufudhu kushiriki mashindano ya Olimpiki yanayotarajia kufanyika mwakani London, Uingereza.

Mashindano hayo ya kufudhu kwa nchi za Afrika yanatarajia kufanyika Aprili 27 mwakani nchini Mexico huku ya kishirikisha wachezaji 66 kutoka Afrika.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema, wameamua kuiweka wazi programu hiyo ili iweze kuchangiwa na wadau wa ngumi na watanzania wote ili kuweza kufanikisha timu ya Taifa kushiriki katika mashindano hayo.

Alisema, ratiba hiyo wanatarajia kuiweka wazi wiki ijayo ili kila mtu aweze kuiona na kuichangia kwa manufaa ya mchezo na Taifa kwa ujumla.

"Tumeamua kufanya hivyo ili iwe rahisi kwa wadau wote kujua nini kinaendelea na pia kuhitaji mchango wao kwani BFT peke yetu hatutaweza kumudu kila kitu kwa timu hivyo kuchangia kwao kutasaidia timu iweze kushiriki katika mshindano hayo," alisema Makore.

Alisema pia, hiyo itasaidia kuepusha lawama kwa BFT ambapo ikifika hadi siku ya mashindano timu ikishindwa kushiriki lawama ziwe kwa nchi nzima nasi kwa BFT pekee kwani timu si ya BFT ni ya nchi.

Alisema, kwa sasa wachezaji wote wapo katika kambi zao wakiendelea kujifua kabla ya kukaa kambi ya pamoja kwa ajili ya mashindano

No comments:

Post a Comment