Wednesday, December 14, 2011

MOTO KUWAKA DDC KEKO DESEMBA 24


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Venance Mponji,a anatarajia kuzichapa na mpinzani wake Chaurembo Palasa, katika pambano la kuwania ubingwa wa TPBC wa Afrika litakalopigwa Desemba 24 mwaka huu katika Ukumbi wa DDC Keko, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam , Promota wa pambano hilo, Kaike Siraji, alisema kuwa wameandaa pambano hilo ili kuweza kumaliza ubishi uliopo kati ya mabondia hao.

Alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa la aina yake kwani mabondia hao wameshakutana mara mbili ambapo kila bondia ameshinda mara moja.

Kaike alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa la uzito wa Light Walter ambalo litakuwa la raundi 12.

Alisema kuwa pia katika pambano hilo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ambayo yatashirikisha mabondia wa uzito tofauti tofauti.

“Tumeandaa pambano la aina yake ambalo litaweza kuondoa ubishi na bingwa wa pambano hilo, nitamtafutia pambano la kimataifa ambapo atazichapa na bondia kutoka New Zealand ambapo pambano hilo litafanyika hapa nchini mapema mwakani” alisema.

Aliwataja mabondia wengine watakaozichapa katika pambano hilo kuwa ni pamoja na Baina Mazora ambaye atazipiga na Juma Fundi katika pambano la uzito wa Bantam la raundi nane, pambano lingine litawakutanisha Seba Temba na Said Zungu litakalokuwa la raundi sita katika uzito wa Light.

Wengine ni Fred Sayuni ambaye atazichapa na mpinzani wake Simba Tunduru katika pambano la uzito wa Bantam la raundi sita na Mainya Ramadhan atapigana na Mikidadi Tyson katika pambano la raundi sita katika uzito wa Light Weight

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D

No comments:

Post a Comment