Sunday, April 22, 2012

Lowassa Atoa Mil. 10 ujenzi wa kanisa Mbeya



Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) akiwa pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT,Askofu Keneth Kasunga katika ibada maalumu wakati wa tafrija ya uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa hilo lililopo mjini Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya,iliyofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya High Class mjini humo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo ya  kuchaangia ujenzi wa Kanisa la EAGT lililopo mjini Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na MC Charles Mwakipesile ambaye pia ni mwandishi wa habari gazeti la Majira mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akiagana na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo.Wa pili Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya,Mh. Evance Balama.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiwapungia waumini wa Kanisa la EAGT mara baada ya kuwahutubia wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa kanisa hilo lililopo mjini Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT,Askofu Keneth Kasunga pamoja na waumini wengine wa kanisa hilo wakati wakitoka kwenye viwanja vya Hoteli ya High Class muda mfupi baada ya hafla fupi ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo,lililopo mjini Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mara baada kumalizika kwa tafrija hiyo.
 
 
Na Mwandishi Wetu,Mbeya.
WAZIRI mkuu mstaafu,Edward Lowassa ametoa Shilingi Milioni 10 taslimu kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la EAGT lililopo mjini Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Fedha hizo amezitoa wakati wa harambee ya kuchagia ujenzi wa kanisa hilo ililofanyika katika viwanja vya Hoteli ya High Class mjini hapa.
Lowassa ambaye alitumia takribani dakika 28 pekee kuwepo katika viwanja hivyo, alisema kuwa watanzania ni vema wakawa na wito wa kujenga nyumba za kuabudia kuliko kujenga nyumba za starehe zikiwemo Bar.
‘’Nafurahi kualikwa katika tafrija hii na niwaombe kwa pamoja tuwe na tabia za kujenga nyumba za Mungu ambazo zitakusanya waumini kuabudia na kuomba kwa pamoja kuliko hivi ilivyo wengi wanajenga Bar’’ alisema Lowassa.
Aliongeza kuwa kwa sasa nchi ipo katika kipindi kigumu cha uchumi na masuala ya katiba mpya hivyo aliwaomba wakristo kupanga ratiba ya kuiombea nchi ili iendelee kuwa na amani na watanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na umoja uliopo.
Alisema kuwa jambo hilo ni muhimu kwa kila mtanzania ambapo kila mmoja aliombee taifa,ili lisikumbwe naghasia na mambo kama yale yanayotokea katika nchi zingine ikiwemo  Nigeria ambako kikundi cha Boko Haramu hakiwataki Wakristo.
‘’Mimi ,familia yangu na marafiki zangu  tumeguswa na ujenzi wa nyumba ya Mungu na tunatoa Shilingi Milioni 10 na huu ni mwanzo tu’’ alisema Lowassa.
Sanjari na kutoa fedha hizo, pia alimuomba askofu wa kanisa hilo aandae tamasha la kuchagia ujenzi huo kwa kwaya zote ambazo zilihudhuria harambee hiyo na kwamba kwaya tatu zitakazoshinda zitachagua mwakilishi mmoja ambao atawagharamia kwenda nchini Israel kuona historia ya kikristo.
Alisema amefanya hivyo kwasababu anapenda sana uimbaji na kwamba alibarikiwa zaidi alipoimba pamoja na wanakwaya hao wimbo usemao ‘’Bwana Mungu nashangaa kabisa nikitazama jinsi ulivyo……..
Kwa upande wake Askofu mkuu wa Kanisa hilo,Keneth Kasunga alimshukuru Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kuwa amejenga nyumba ya Mungu na wala si ya Mtu binafsi hivyo Mungu hawezi kumuacha katika mambo yake yote na mahitaji pia.
Kanisa hilo lilisema kuwa katika ujenzi wa kanisa hilo lenye waumini 750, walipungukiwa kiasi cha Shilingi Milioni 750, kanisa litakaloweza kuwaondolea adha waumini ambao wanasali wakiwa nje kutokana na kanisa lililopo kwa sasa kuwa dogo.

No comments:

Post a Comment