Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Epraim Mafuru
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
wakati wa uzinduzi rasmi wa Promotion ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO
kupitia bia tatu za Serengeti, Tusker na Pilsner Lager na washindi
kujizolea zawadi mbali ambapo zawadi za Shilingi Milioni 700
kushindaniwa. Pamoja nae Kulia ni Mkuzaji wa M PESA kutoka Kitengo cha
Biashara, Asia Natalia Mhina na Kushoto ni Meneja wa Bia ya Pilsner
Lager, Maurice Njowoka.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Epraim Mafuru (katikati)
akionesha zawadi mbali mbali zitakazo tolewa katika Promotion hiyo ya
VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO kupitia bia tatu za Serengeti, Tusker na
Pilsner Lager na washindi kujizolea zawadi mbali ambapo zawadi za
Shilingi Milioni 700 kushindaniwa. Zawadi zitakazo tolewa ni pamoja na
Fedha Taslimu, Bia za Bure, Jenereta, Bajaji, Pikipiki na Gari aina ya
Figo. Mafuru amesema Promosheni hii itadumu kwa Wiki 16 kuanzia Jumanne
Aprili 24,2012.
Kulia ni Mkuzaji wa M PESA kutoka Kitengo cha Biashara, Asia Natalia Mhina.
****
Kampuni
ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia vinywaji vyake bora kabisa vya
Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager iameandaa
promosheni kubwa na ya aina yake itakayofanyika Tanzania nzima katika
kipindi cha wiki 16 ambapo zawadi mbalimbali zitashindaniwa.
Promosheni
hiyo ya aina yake imesheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile
Jenereta 16 , Pikipiki 8, Bajaji 8, Gari ndogo maarufu kama saloon car
8, pamoja na zawadi zingine nyingi ambapo kila baada ya wiki mbili gari 1 aina ya saloon itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki mbili Bajaji 1 itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki Pikipiki moja itashindaniwa na kila baada ya wiki moja Jenereta moja itakuwa inashindaniwa.
Akizungumzia promosheni hiyo kabambe Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, bwana Ephraim Mafuru amesema promosheni
hiyo sio tu inalenga kuongeza mauzo ya vinywaji hivyo bali pia inalenga
kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa
zinazozalishwa na kampuni hiyo ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hiyo
kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora wa
aina yake.
“Kampuni
yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya taifa letu
katika maeneo mbalimbli kupitia jamii inayotuzunguka na wateja wetu
kimaisha, hivyo promosheni hii pamoja na ukweli kuwa inalenga kuongeza
tija katika masoko ya bidhaa zetu bado unaweza kuona zawadi
zitakazoshindaniwa katika promosheni hii ni zawadi kubwa ambazo kwa
namna moja ama nyingine inaweza kubadilisha maisha ya mshindi wetu
kutoka hatua aliokuwepo hadi hatua nyingine, kwa hivyo sisi SBL tunasema
tunajivunia kuwa sehemu mojawapo inayochangia maendeleo ya watanzania
wateja wetu na taifa kwa ujumla” alisema bwana Mafuru.
Kwa
upande wake Meneja wa bia ya Tusker Lager, Bi Rita Mchaki, amesema
kampuni ya bia ya Serengeti inazalisha bidhaa zinazopendwa na watanzania
wengi kutokana na ubora wa kipekee wa bidhaa hiyo, na kwamba promosheni
hiyo kabambe nisawa nakurudisha shukrani zake kwa watanzania kwa
kufanikisha kampuni hiyo kufikia malengo yake kibiashara.
Watanzania
wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi na wanaotumia bidhaa zetu
zilizoainishwa katika promosheni hii wanaombwa kushiriki kwa wingi bila
kukata tamaa kwani zawadi zinazoshindaniwa zinaweza kubadilisha maisha
kwa yeyote atakayebahatika kuibuka na ushindi.
MAELEKEZO:
Nunua
bia ya serengeti lager, Tusker lager au Pilsner Lager fungua kisha
bandua ganda lililo ndania ya kizibo utapata namba zilizopo katikati ya
kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako, nakili
namba hizo mfano 55550, kisha tuma namba zilizopo pembezoni mwa
kizibo. Fanya hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na
magazeti.unaweza pia kijipatia bia ya bure papo hapo kila ubanduapo
kizibo cha bia ziliainishwa katika promosheni hii.
No comments:
Post a Comment