Wawakilishi
pekee waliobaki toka Klabu za Tanzania katika michuano ya Barani
Afrika, Simba, leo wanatinga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza
Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya michuano ya CAF ya
Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Al Ahly Shandy ya Sudan.
Katika
Raundi zilizopita, Simba walibwaga Kiyovu ya Rwanda kwa jumla mabao 3-2
katika Mechi mbili kisha kuwatoa ES Setif ya Algeria kwa bao la ugenini
baada ya kufungana bao 3-3 katika Mechi mbili, Simba wakishinda Dar es
Salaam bao 2-0 na kuchapwa 3-1 huko Mjini Setif, Algeria.
Nao
Al Ahly Shandy waliwatoa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji Raundi
iliyopita na ingawa Klabu hii ya Sudan ni mara ya kwanza kucheza
michuano ya Klabu Afrika lakini kwa mchezo ilioonyesha walipocheza na
Ferroviario de Maputo na kushinda 1-0 ugenini Maputo na 2-0 kwenye Mechi
ya marudiano, Timu hii si ya kubeza.
Timu
hizi zitarudiana hapo Jumamosi Mei 12 huko Mjini Shandy, Mji ambao uko
Kilomita 150 Kaskazini Mashariki ya Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum.
Na katika mechi hiyo kiingilio cha chini ni sh 5,000/=
Na katika mechi hiyo kiingilio cha chini ni sh 5,000/=
No comments:
Post a Comment