Saturday, May 12, 2012

CHANETA WABOA ILE MBAYA, AZZAN AMALIZIA HASIRA KWENYE KULAMBA HII KITU



Pichani ni Mbunge wa Kinondoni, Iddi Mohamed Azzan, mmoja wapenzi wa michezo waliohudhuria mechi hiyo- hapa akipoza koo kwa bidhaa ya Azam baada ya kusubiri sana.  

MECHI ya mwisho ya mashindano ya Afrika ya Netiboli yanayofikia tamati leo Dar es Salaam, kati ya wenyeji Tanzania na Botswana inatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa katika Uwanja wa Taifa.
Mechi hiyo iliyokuwa ianze saa 7:30 mchana, Uwanja wa Taifa wa nje, ilichelewa kuanza kutokana na mvua kali, hivyo kuhamishiwa Uwanja wa ndani.
Hata hivyo, Uwanja wa ndani nako kukawa hakuna umeme, hivyo zikafanyika jitihada za kuwasiliana na TANESCO warejeshe umeme eneo hilo, ambazo zimezaa matunda dakika kama 30 zilizopita.
Mgeni rasmi, mke wa makamu wa rais, mama Bilal na mke wa Waziri Mkuu mama Pinda hawajafika bado ukumbini. Lakini kwa ujumla, CHANETA imewaangusha mno wadhamini wao, Serengeti Breweries Limited (SBL), Vodacom na Coca Cola pamoja na wadau wengine waliochangia kwa kuhamasishwa na Mama Tunu Pinda kutokana na ubabaishaji huu.
Hawakuwa na maandalizi ya kutosha- hawakuwa na maamuzi ya haraka. Kwa ujumla, wamejitengenezea mazingira ya kunyimwa udhamini siku za usoni.
Tanzania ikishinda itakuwa mshindi wa pili, wakati Malawi tayari wametetea ubingwa wao kwa kushinda mechi zote.http://bongostaz.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment