Pichani ni Mbunge wa Kinondoni, Iddi Mohamed Azzan, mmoja wapenzi wa michezo waliohudhuria mechi hiyo- hapa akipoza koo kwa bidhaa ya Azam baada ya kusubiri sana. |
MECHI ya mwisho ya mashindano ya Afrika ya
Netiboli yanayofikia tamati leo Dar es Salaam, kati ya wenyeji Tanzania na
Botswana inatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa katika Uwanja wa Taifa.
Mechi hiyo iliyokuwa ianze saa 7:30 mchana,
Uwanja wa Taifa wa nje, ilichelewa kuanza kutokana na mvua kali, hivyo kuhamishiwa
Uwanja wa ndani.
Hata hivyo, Uwanja wa ndani nako kukawa
hakuna umeme, hivyo zikafanyika jitihada za kuwasiliana na TANESCO warejeshe
umeme eneo hilo, ambazo zimezaa matunda dakika kama 30 zilizopita.
Mgeni rasmi, mke wa makamu wa rais, mama
Bilal na mke wa Waziri Mkuu mama Pinda hawajafika bado ukumbini. Lakini kwa
ujumla, CHANETA imewaangusha mno wadhamini wao, Serengeti Breweries Limited (SBL),
Vodacom na Coca Cola pamoja na wadau wengine waliochangia kwa kuhamasishwa na
Mama Tunu Pinda kutokana na ubabaishaji huu.
Hawakuwa na maandalizi ya kutosha- hawakuwa
na maamuzi ya haraka. Kwa ujumla, wamejitengenezea mazingira ya kunyimwa
udhamini siku za usoni.
Tanzania ikishinda itakuwa mshindi wa pili,
wakati Malawi tayari wametetea ubingwa wao kwa kushinda mechi zote.http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment