Afisa
Uhusiano wa Maxinsure akiongea na waandishi wa habari walipoenda
kukabidhi misaada katika hospitali ya Tumbi, kushoto kwake ni Mganga
mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk. Issac Lwari
Afisa Uhusiano wa Maxinsure akionyesha mashuka alioyakabithi katika hosptali ya Tumbi hivi karibuni
Meneja
Madai wa Kampuni ya Maxinsure ,Bw. Ian Kifunta akishikilia mashuka ya
msaada wakati walipokua wanatembelea hospitali ya Tumbi hivi karibuni
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk Issach Lwari akiwaonyesha wafanyakazi wa
Maxinsure mashine mbovu,iliyokua ikinyooshea nguo za hospitalini hapo.
Hospitali
ya Tumbi ya mjini kibaha yapokea msaada wa mashuka 50 yenye thamani ya
shillingi za kitanzania 500,000 kutoka katika kampuni ya Bima ya
Maxinsure hivi karibuni, Msaada huo ukiwa umetokana na na taaarifa
iliyotoka katika gazeti maarufu moja nchini,likiwa linaelezea kuhusu
upungufu wa mashuka katika hospitali hiyo.
Kampuni
ya Maxinsure ndio imekua kampuni ya kwanza kabisa nchini kuitikia wito
huo, huku Bima kuu ya Afya ya nchini ikihahidi kutoa mashuka pia hivi
karibuni.
“Tunashukuru
sana kampuni ya Maxinsure kwa kuguswa na tatizo letu,tunategemea kupata
mashuka zaidi na tunaomba makampuni mengine yaweze kujitokeza
kutusaidia, kwani hili sio tatizo pekee linaloikabili hospitali
yetu”.Alisema Mganga mkuu wa hospitali ya Tumbi,Dk.Issach Lwari
akishukuru kwa msaada alioupokea
Kwasasa Hospitali ya Tumbi ina mashuka yapatayo 900 huku ikiwa bado na uhitaji wa mashuka yasiopungua 1,124.
DK.
Lwari alitaja matatizo mengine kama ,mashine za kufulia, upungufu wa
damu na pia hospitali iyo inakabiliwa na ukosefu wa Vipimo mbalimbali
,swala linalopelekea kuwashauri wagonjwa wachukue vipimo katika
hospitali nyingine
No comments:
Post a Comment