JK AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IVORY COAST JIJINI ARUSHA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast
wakitembea kwa miguu kuelekea kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia
mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo Mei 30,
2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB
ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC.
Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi
za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB
ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya
uchaguzi mkuu mwaka jana.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast
wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea kwenye sehemu
waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini
Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika
kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais
Kikwete katika ukumbi wa AICC.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast
wakiwa katika mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha
leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria
mkutano wa afDB ambao unafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika
ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania
inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo
makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu
zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment