Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 25, 2012

HALI BADO TETE YANGA LICHA YA NCHUNGA KUJIUZULU



KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Yanga kujadili barua ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga kujiuzulu kimeshindwa kufanyika leo, kutokana na safu kutotimia.
Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, Mbaraka Igangula yupo Afrika Kusini wakati Khalifa Mgonja yupo Arusha,
Mwesigwa alisema kwa sababu hiyo, wanasubiri Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji wafike Dar es Salaam ndipo kikao kifanyike. Wakati huo huo, Wazee wa klabu hiyo walikutana na waandishi wa Habari leo mchana makao makuu ya klabu na kusema kwamba, hawamtambui Mjumbe yeyote wa Kamati ya Utendaji, kwani Nchunga ameondoka na watu wake wote.
Aidha, baadhi ya Wajumbe waliotangaza kujiuzulu wameanza kuzikana barua zao, wakidai walilazimika kuandika kutokana na vitisho walivyokuwa wakipewa.  BIN ZUBEIRY iliwasiliana na Mwanasheria wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alex Mgongolwa kutaka ufafanuzi zaidi juu ya sakata la klabu hiyo, lakini akasema yuko kwenye kikao.
Wakati BIN ZUBEIRY ikiwa imetega rada zake kwa Mgongolwa hadi hapo atakapomaliza kikao, taarifa zaidi zinasema kikao hicho kinahnusu syala hilo hilo la Yanga na atalitolea tamko leo.
Jana, Nchunga alitangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Yanga, akisema timu anaikabidhi kwa Baraza la Wadhamini, ambalo kwa sasa linaundwa na wajumbe watatu, Mama Fatuma Karume, Deo Filikunjombe na Francis Kifukwe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...