Drogba akishangilia bao la kusawazisha. |
Gomez akiruka kuwania mpira na kipa wa Chelsea. |
Bayern wakishangilia bao la kuongoza, kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Didie Drogba. |
Kipa wa Bayern akiuchungulia mpira uliopigwa na Drgoba, wakati ukitinga wavuni na kuandika bao la kusawazisha. |
TIMU
ya Chelsea jana usiku iliwashangaza mashabiki wa Soka duniani pale
ilipotwaa ubingwa na Kombe la Mabingwa Ulaya, baada ya kuifunga Bayern
Munich kwa penalti 4-3 baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1
katika dakika 120, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena,
Munich, Ujerumani.
Nyota
wa mchezo huo wa jana Didier Drogba, ambaye aliisawazishia timu yake
bao muhimu katika mchezo huo katika dakika za majeruhi na kusababisha
penati, pia ndiye aliyeweza kuwainua mashabiki wa timu hiyo kote
Duniani pale alipokwenda kupiga penati ya mwisho ambayo ilikuwa ni
muhimu na yenye Presha lukuki.
Kwani iwapo angekosa penati hiyo timu hizo zingerejea katika upigaji wa penati moja moja tena hadi apatikane mshindi.
Katika
ushindi huo muhimu pia Kipa wa Chelsea, Petr Cech, aliyeweza kuokoa
penati mbili za Bayern sifa zimuendee kipa aliyecheza penalti mbili za
Bayern.
Wengine
waliofunga penati za Chelsea ni David Luiz, Frank Lampard na Ashley
Cole, huku penati ya Juan Mata ikiokolewa na kipa wa Bayern Neur.
Nao Bayern, waliofunga ni Lahm, Gomez na kipa Neur.
No comments:
Post a Comment