Monday, May 21, 2012

CHELSEA YATWAA TAJI LA MABINGWA WA ULAYA KWA KUWACHAPA BAYERN KWA PENATI 4-3


Drogba akishangilia bao la kusawazisha.
Gomez akiruka kuwania mpira na kipa wa Chelsea.
Bayern wakishangilia bao la kuongoza, kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Didie Drogba.
Kipa wa Bayern akiuchungulia mpira uliopigwa na Drgoba, wakati ukitinga wavuni na kuandika bao la kusawazisha.

TIMU ya Chelsea jana usiku iliwashangaza mashabiki wa Soka duniani pale ilipotwaa ubingwa na Kombe la Mabingwa Ulaya, baada ya kuifunga Bayern Munich kwa penalti 4-3 baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya  1-1 katika dakika 120, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Munich, Ujerumani.

Nyota wa mchezo huo wa jana  Didier Drogba, ambaye aliisawazishia timu yake bao muhimu katika mchezo huo katika dakika za majeruhi na kusababisha penati, pia ndiye aliyeweza kuwainua mashabiki wa timu hiyo kote Duniani pale alipokwenda kupiga penati ya mwisho ambayo ilikuwa ni muhimu na yenye Presha lukuki.

Kwani iwapo angekosa penati hiyo timu hizo zingerejea katika upigaji wa penati moja moja tena hadi apatikane mshindi. 

Katika ushindi huo muhimu pia Kipa wa Chelsea, Petr Cech, aliyeweza kuokoa penati mbili za Bayern sifa zimuendee kipa  aliyecheza penalti mbili za Bayern.
Wengine waliofunga penati  za Chelsea ni David Luiz, Frank Lampard na Ashley Cole, huku penati ya  Juan Mata ikiokolewa na kipa wa Bayern Neur.  

Nao Bayern, waliofunga ni Lahm, Gomez na kipa Neur.

No comments:

Post a Comment