Participants to a one-day Airtel Rising Stars directive
seminar take part in a brief warm up during a one-day directive seminar held in
Dar es Salaam
over the weekend to guide school sports masters and regional football
administrators on rules and regulations governing the U-17 Airtel Rising Stars
tournament.
Usajili
wa wachezaji kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2012 inatarajiwa kufikia tamati Jumatano, Mei
23 kwa mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha, Mbeya na Aruhsa.
Jumla ya timu 24 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ngazi ya miaka na
hatimaye ngazi ya Taifa itakayofanyika mwezi Julai Jijini Dar es Salaam
Mikoa
shiriki ilichanguliwa kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano ya Taifa ya
Shule za Sekondari (UMISSETA) iliyoisha hivi karibuni. Uzinduzi rasmi wa Airtel
Rising Stars 2012 ulifanyika hivi karibuni chini ya mchezaji wa zamani wa Manchester United ya Uingereza, Quinton Fortune kwenye
Hoteli ya Sea Cliff, Dar es Salaam .
Michuano
ya Airtel Rising Stars 2012 ina umuhimu wa kipekee kwa kuwa timu sita za
wasichana zitashiriki kwenye ngazi ya Taifa. Akiongea kuhusu wasichana
kushiriki kwenye michuano hii, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Cheikh Sarr
alisema, ‘Airtel imeamua kujumuisha wasichana kwenye michuano hii kuwapa nafasi
ya kuendeleza vipaji vyao na pia kuipa Timu ya Taifa ya wanawake ya Twiga Stars
wasaa wa kupata vipaji vipya.
Wakati
wavulana wakitarajiwa kushindana kuanzia ngazi ya mkoa ili kuchanguliwa kupata
nafasi ya kucheza Taifa, timu moja ya wasichana kutoka kila mkoa itashiriki
moja kwa moja fainali za Taifa na hivyo kufanya timu 12 kushiriki, ngazi hii, sita
wavulana na sita wasichana.
Akizungumzia
juu ya Airtel Tanzania
kuwekeza kwenye soka, Cheikh Sarr alisema ‘ Tunajisikia furaha kukuza vipaji
vidogo kuanzia ngazi ya chini kabisa, huu ndio muda kila mtu alikuwa
akiisubiri.’ Ni muda muafaka kwa Tanzania kuzalisha stars wake –
aliongeza Sarr.
Michuano
ya ARS ngazi ya mkoa inarajiwa kuanza Mei 25, huku Dar es Salaam ikiwa na timu sita kutoka
Kinondoni, Ilala na Temeke. Shule hizo ni Twiga, Goba na Makongo Sekondari
(Kinondoni) Mbande, Kurasini na Kiravi Sekondari (Temeke) huku Ilala ikiwakilisha
na Airwing, Benjamin Mkapa na Msongola Sekondari.
Shule
zingine zitakazoshiriki kwenye michuano hii ni Southern Highland Sekondari,
Mbeya High na Wenda Sekondari (Mbeya), Lindi Sekondari, Mpunyule na Ngowe
Sekondari (Lindi) huku Arusha ikiwakilisha na Sinoni Sekondari, Kaloleni na
Bishop Durning Sekondari.
Michuano
wa Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa kutafuta
na kukuza vipaji vya soka vinavyochipukia kwa wavulana na wasichana wenye miaka
chini ya kumi na saba ambao watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na
wataalamu wa mpira wa miguu ambao watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya
kukuza vipaji vyao.
Airtel
Rising Stars ni ushirikiano kati ya Airtel na klabu ya Uingereza ya Manchester United ya
kukuza vipaji vya soka barani Afrika. Mwaka jana, Klabu ya Manchester United
ilitoa walimu wake wa soka ya vijana kuendesha kliniki ya soka ya Kimataifa
ambazo kliniki hizo zilifanyika Tanzania ,
Afrika Kusini na Gabon .
Kliniki
ingine kama hiyo itafanyika
No comments:
Post a Comment